Search This Blog

Loading...

Friday, May 17, 2013

RONALDO NA MOURINHO WAMALIZA MSIMU KWA AIBU YA KUTOLEWA NJE YA UWANJA - REAL MADRID WAKIFUNGWA NA ATLETICO MADRID KWENYE FAINALI YA COPA DEL REY


Copa del Rey Final: Real Madrid 1-2 Atletico... by ourmatch
Mourinho sent off by Counterpoint1
CR7 Red by Counterpoint1

BAYERN MUNICH VS DORTMUND: WIKI KABLA YA FAINALI DORTMUND WAWAKUMBUSHA BAYERN MACHUNGU YA GOLI LA SOLSKJAER

Oh no you di'int, Dortmund! (101GG)

Huku zimebakia siku chache kabla ya fainali yao ya Champions League dhidi ya Bayern Munich ndani ya dimba la Wembley, Borussia Dortmund wameanza mind games kwa kuwakumbusha Mabavarian moja ya kumbukumbu zao mbaya kabisa za fainali ya UCL.
BVB wameweka jezi ya Manchester Utd iliyokuwa ikivaliwa na  Ole Gunnar Solskjaer katika jumba lao la makumbusho. Hii itawakumbusha Bayern Munich alichowafanya Mnorway huyo alipofunga goli la ushindi katika dakika ya 93 ya mchezo katika fainali ya mwaka1999 ya Champions League. Tukio hili limekuwa moja ya muhimu katika historia ya michuano hiyo.

Jezi hiyo ni ya Ole Gunnar Solskjaer sio ile aliyoivaa kwenye fainali ya mwaka 99, hii ni ile ambayo alivaa kwenye mchezo wa nusu fainali ya European Cup dhidi ya Dortmund ambapo United walifungwa na Solskjaer - Baby-Faced Assassin alibadilishana na jezi na Knut Reinhard.

KALI YA LEO: MOURINHO AGOMA KWENDA KWENYE MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI - MWANDISHI AMALIZIA HASIRA ZAKE KWENYE PICHA YAKE


Jose Mourinho hakutokea kwenye mkutano wa waandishi wa habari siku moja kabla ya mchezo wa fainali wa Copa del Rey baina ya Real Madrid na Atletico Madrid, hivyo Sergio Ramos aliachwa kujibu maswali ya waandishi mwenyewe. Mwandishi mmoja wa kibrazil hakuridhishwa na suala la Mourinho kutotokea hivyo akaamua kuonyesha hasira zake kwa kuchana chana picha ya Mourinho.

Mwandishi huyo alikuwa akichana picha huku akisema kwamba kocha huyo wa kireno ni mpumbavu.

EXCLUSIVE: HIZI NDIO ORODHA MBILI ZA MAREFA WALIOPANGWA KUCHEZESHA MECHI ZA MWISHO ZA LIGI KUU - KABLA NA BAADA YA KUBADILISHWA NA TFF - MWAMUZI WA MCHEZO WA WATANI TU NDIO ABADILISHWA

Hii ndio orodha ya marefa watakaochezesha mechi za mwisho za ligi kuu kabla ya kubadilishwa kwa mwamuzi mmoja tu wa mchezo wa Simba vs Yanga.


Hii ndio orodha ya pili ilitolewa na TFF baada ya kumbadilisha refa wa mchezo wa Simba na Yanga huku mechi nyingine kukiwa hakuna mabadiliko yoyote ya waamuzi.



PAZIA LA LIGI KUU YA VODACOM LAFUNGWA KESHO - TIMU ZOTE 14 DIMBANI

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu (2012/2013) inafikia tamati kesho (Mei 18 mwaka huu) kwa timu zote 14 kupambana katika viwanja saba tofauti.

Mechi zote zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Ni jukumu la kamishna wa mechi husika kuhakikisha mchezo unaanza katika muda uliopangwa, vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom toleo la 2012.

Yanga ambayo tayari imeshatwaa ubingwa itakuwa mgeni wa Simba katika mechi namba 180 itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo mwamuzi atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro na Kamishna ni Emmanuel Kavenga wa Mbeya.

Mgambo Shooting vs African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mwamuzi ni Amon Paul wa Mara wakati Kamishna ni Ally Mkomwa kutoka Pwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Mwamuzi ni Israel Mujuni wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Salum Kikwamba kutoka Kilimanjaro).

Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mwamuzi ni Ibrahim Kidiwa wa Tanga wakati Kamishna ni John Kiteve kutoka Iringa), Oljoro JKT vs Azam (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha. Mwamuzi ni Athuman Lazi wa Morogoro wakati Kamishna ni Juma Mgunda kutoka Tanga).

Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro utatumika kwa mechi kati ya Polisi Morogoro na Coastal Union ya Tanga ambapo Mwamuzi atakuwa Said Ndege wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Hakim Byemba kutoka Dodoma. Toto Africans itacheza na Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mwamuzi ni Geoffrey Tumaini kutoka Dar es Salaam na Kamishna ni Josephat Magazi wa Singida.

MECHI ZA MARUDIANO RCL WIKIENDI HII
Mechi za marudiano za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zinachezwa wikiendi hii katika viwanja kumi tofauti wakati mechi ya Flamingo ya Arusha na Machava FC ya Kilimanjaro yenyewe itachezwa Jumatatu (Mei 20 mwaka huu).

Uamuzi wa mechi hiyo kuchezwa Jumatatu ni kutokana na Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid kutumika kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kesho wakati Jumapili utatumika kwa shughuli nyingine za kijamii kwa mujibu wa wamiliki wa uwanja huo (CCM Mkoa wa Arusha).

Mechi nyingine zitachezwa keshokutwa (Jumapili) ambapo Abajalo watakuwa wenyeji wa Red Coast kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara utatumika kwa mechi kati ya wenyeji Coast United na Kariakoo ya Lindi.

African Sports ya Tanga itaoneshana kazi na Techfort ya Ifakara mkoani Morogoro katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani. Nayo Simiyu United ya Simiyu itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua, mjini Singida.

Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ndiyo utakaotumika kuzikutanisha timu za Polisi Jamii Bunda kutoka Mara na wenyeji UDC wakati Biharamulo FC ya Kagera na Polisi SC ya Geita zitaumana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Milambo FC ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Saigon FC ya Kigoma kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora huku Mbinga United ya Ruvuma ikiikaribisha Njombe Mji ya Njombe kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa utatumika kwa mechi kati ya wenyeji 841 KJ dhidi ya Kimondo SC kutoka Mbeya. Nazo Rukwa United na Katavi Warriors zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya pili zitacheza mechi zao za kwanza kati ya Mei 25 na 26 mwaka huu wakati mechi za marudiano ni kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

PICHA YA SIKU: WOTE WAMESTAAFU KASORO BABU GIGGS



Thursday, May 16, 2013

MABAO BORA YA DAVID BECKHAM YAKIWEMO 85 ALIYOIFUNGIA MANCHESTER UNITED

VIDEO: DAVID BECKHAM AKIHOJIWA NA GARY NEVILLE KUTANGAZA UAMUZI WAKE WA KUSTAAFU

EXCLUSIVE: SIMBA NA YANGA - BILA MILLIONI 100 HATUTAKI MECHI YETU IONYESHWE NA KITUO CHOCHOTE CHA TV

Wakati ikiwa imebaki siku moja kabla ya mtanange wa tani wa jadi Simba na Yanga kufanyika huku kukiwa na taarifa kwamba mchezo huo unaweza kuonyeshwa kwenye moja ya kituo cha TV, leo hii viongozi wa klabu hizo mbili wamezungumza exclusively na mtandao huu kuhusiana na mchezo wa timu zao kurushwa moja kwa moja na kituo chochote cha Television.

Awali shirikisho la soka nchini kwa pamoja na kituo cha SuperSport cha Afrika Kusini lilikuwa na utaratibu wa kile kilichoitwa SUPER WEEK ambapo baadhi ya mechi hizo zingeonyeshwa live kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Lengo la SuperSport la kuonyesha mechi hizo live ni ‘kuipromoti’ ligi ya Tanzania na wachezaji wake ili waweze kupata kuonekana na watu wengine na kuingia katika biashara nzuri ya soka. 


Lakini viongozi wa vilabu vya ligi kuu waligoma mechi hizo kuonyeshwa bila wao kupata malipo hivyo mpango huo ukafa bila majibu ya kujitosheleza.

Lakini leo zimeibuka taarifa kwamba kituo hicho na shirikisho wapo katika hatua za kutaka mechi hiyo ya watani wa jadi ionyeshwe live.

Wakiongea na mtandao huu Ktibu Mkuu wa Simba Mtawala na makamu mwenyekiti wa Clement Sanga walisema: "Ikiwa kama  kama kuna mpango huo TFF wakae watambue kwamba hatutokubali mechi yetu ionyeshwe bure. Ni wakati sasa tupate kile tunachostahili sio kuwaingizia watu wengine fedha wasizostahili. Tamko letu la pamoja tunasema kwamba ikiwa kuna kituo chochote kinachotaka kurusha mechi yetu basi kitoe Millioni 100 - millioni 50 kwa kila timu na si vinginevyo. Ikiwa hakuna atakayeweza kufikia kulipa fedha hizo basi mechi yetu haitoonyeshwa na kituo chochote cha TV."

BAADA YA FERGIE NA SCHOLES - DAVID BECKHAM NAE ATANGAZA KUSTAAFU SOKA MWISHONI MWA MSIMU HUU

Kustaafu ndio habari iliyoshika hatamu nchini Uingereza hiv sasa - wiki moja baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, Paul Scholes, leo hii mchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa England DAVID BECKHAM ametangaza kutundika daluga.

Beckham, 38, ameisadia Paris Saint-Germain kubeba kombe la  Ligue 1 kwa mara ya kwanza ndani miaka 19 mwishoni mwa wiki hii.
Pamoja na kupewa ofa ya mkataba mpya na timu hiyo ya Ufaransa, mkongwe huyo atastaafu baada ya mchezo wa mwisho tarehe 26 mwezi huuA.
Alisema: “Shukrani sana kwa PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwa hapa lakini sasa nadhani ni muda sahihi wa kustaafu, kucheza kwenye soka la kiwango cha juu
Becks alianza kucheza akiwa na Manchester United, akifunga mabao 85 katika mechi 394, kabla ya kuhamia Real Madrid.
Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007 pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan wakati akiwa kwenye Major League Soccer.

MAKALA: UTITIRI WA TIMU ZA JESHI LIGI KUU UTAZAMWE UPYA - FIFA HAIZITAKI KAMATI YA LIGI YAZILEA


KLABU mbili kongwe za Simba na Yanga ndizo zimetawala soka kwa miaka mingi na wapenzi nchini wamegawanyika katika timu hizo.
Shabiki wa soka anaweza kudai ni mpenzi wa Azam lakini ukweli ama yuko Simba au Yanga. Vile vile, atakayesema ni mpenzi wa Ashanti ndani kuna u-Simba au u-Yanga.
Pamoja na Simba na Yanga kuteka mashabiki wa soka nchini, klabu zinazomilikiwa na majeshi ndizo zinanogesha Ligi Kuu ya Bara inayomalizika keshokutwa. Ligi inashirikisha timu 14 msimu huu ambazo ni; JKT Oljoro, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Mgambo JKT, Prisons, Polisi Morogoro, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Azam FC, Simba, Yanga, African Lyon, Coastal Union na Toto African.

TIMU SITA ZA JESHI LIGI KUU, HAZIONYESHI USHINDANI LAKINI ZA WENZETU NI BALAA
JKT RUVU

Timu sita kati ya hizo zinamilikiwa na majeshi. Jeshi la Polisi lina (Polisi Morogoro) na Magereza (Prisons) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linamiliki nne ambazo ni JKT Oljoro, JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Mgambo JKT.
Kwa tathmini yangu, tofauti na timu za majeshi kutoka nchi nyingine za Afrika hasa kutoka Afrika Kaskazini na Magharibi, ushiriki wa timu za majeshi ya Tanzania ni wa wastani katika ligi kiasi cha kutoweka hamasa ya kutosha ya ushindani. Miaka yote zimekuwa zikishika nafasi za katikati.
Azam FC, klabu inayomilikiwa na kampuni ya S.S.Bakhressa safari hii ilishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo baada ya kuitoa Al Nasri Juba katika raundi ya awali ilikumbana na timu ya Barrack Young Controllers ya Liberia ambayo inamilikiwa na jeshi la nchi hiyo. Azam ilitoka jasho kuitoa timu hiyo kwa mabao 2-1 na kuvuka hatua hiyo.
Hatua iliyofuata Azam ikapangiwa timu nyingine ya jeshi ambayo ni Association Sportive des Forces Armées Royales yaani FAR Rabat ya Morocco. Ulikuwa muziki ‘mnene’. Azam ililazimishwa sare ya bila kufungana na kisha ikatolewa mjini Rabat kwa 2-1.
Ukitazama kwa haraka, utaona timu zinazomilikiwa na jeshi kutoka nchi za Morocco, Algeria, Misri na Libya si nyingi katika ligi husika na nguvu kubwa ya maandalizi inakuwa ya kutosha tofauti na hapa nchini. Hali ni tofauti nchini.
JKT ina timu nne katika ligi kuu, pia ina timu katika Ligi Daraja la Kwanza zinazopambana kupanda daraja huku Polisi ikiwa na timu moja na mlolongo wa timu za daraja la kwanza. Hata Prisons nayo ina timu katika madaraja ya chini.
Mtigwa Sugar na Kagera Sugar ni timu ndugu zote zinalikiwa na kampuni ya Superdoll Group of Companies. Ushiriki wa timu hizo si haba.
Mlolongo huu wa timu zinazomilikiwa na kampuni moja au jeshi moja au mfadhili mmoja, ndio unazifanya taasisi hizi za serikali kushindwa kupata huduma nzuri kutoka kwa wamiliki wake ili kuwa na ushiriki wenye tija katika michuano hiyo.
JKT haiwezi kuzihudumia ipasavyo timu zake kuhimili ushindani kutoka kwa timu zenye nguvu ya fedha kama Simba, Yanga na Azam.

FIFA HAIZITAKI TIMU HIZO, TFF, KAMATI YA LIGI YAZILEA

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeona tatizo hilo na limeagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liangalie uwezekano wa kupunguza utitiri huo ili zisiathiri matokeo.
Kwa mfano sasa Mgambo inahitaji pointi moja tu ili iweze kubaki ligi kuu, tazama imecheza mechi mbili dhidi ya Simba na Azam na kufungwa mechi zote kwa mabao 3-1 na 3-0.
Kamati ya Ligi imejitahidi kupanga ratiba mechi za mwisho timu ndugu zisikutane, lakini zilipokumbana zenyewe katikati ya ligi hali ilikuwaje. Mechi za mwisho Mgambo itamaliza na African Lyon, Toto itakwaana na Ruvu, JKT Ruvu na Mtibwa Sugar, Prisons na Kagera Sugar, JKT Oljoro na Azam na Polisi itakuwa mwenyeji wa Coastal Union.
Ofisa mmoja wa JKT anayeshughulikia michezo anasema hilo la kuwa na timu moja katika ligi na kuiandaa kikamilifu hata wao wameliona lakini vyama vya soka vya mikoa ndivyo vinavyozing’ang’ania timu zao.
“Kwa mfano ukitaka Oljoro uivunje, Chama cha Soka Arusha (ARFA) kitakwambia hakitaki na wanahitaji timu ya ligi kuu na ukitishia kutoihudumia watakwambia wapo tayari kuihudumia. Hata mikoa mingine hali ni hiyo hiyo.
“Timu hizi zinakuwa zetu zikiwa madaraja ya chini lakini zikifika madaraja ya juu vyama vya soka vinazing’ang’ania kuwa nazo. Hatuwezi kukataa kuwa na timu kwani michezo ni miongoni mwa vitu tunavyovipa kipaumbele jeshini,” anasema ofisa huyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia anasema; “Ni kweli hizo timu zipo na hata Fifa hairuhusu timu mbili zinazomilikiwa na taaasisi moja kushiriki ligi kuu.”
“Kutokana na mazingira yetu ya soka hasa suala la kiuchumi, sisi tumeruhusu timu hizo kucheza ligi lakini tukiziangalia kwa karibu huku tukibana mazingira ya kupanga matokeo kuanzia katika ratiba na mambo mengine,” anasema.
Ligi Kuu ya Bara inafikia tamati keshokutwa Jumamosi huku Yanga itakayokwaana na Simba ikiwa imeshatwaa ubingwa baada ya kujikusanyia pointi 57.
MAKALA HII IMECHOTWA KATIKA GAZETI LA MAWIO IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI

SIMBA VS YANGA: - KUJIAMINI KUNAWEZA KUKAIGHARIMU YANGA DHIDI YA WATANI WAO WA JADI

GUMZO lililotawala medani ya soka nchini ni pambano la funga dimba ya Ligi Kuu ya Bara litakalowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo itafanyika huku Yanga ikiwa tayari imeshatwaa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 57 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki michuano hiyo. Mchezo huu utakuwa wa kulinda heshima tu kwani Simba haiwezi hata kutwaa nafasi ya pili.
Mashabiki wa Yanga wamejiaminisha kwamba mechi hiyo itakuwa ya kulipa kisasi cha kipigo cha mabao 5-0 ambacho ilikipata katika mechi ya mwisho msimu uliopita. Yanga wanajipa imani hiyo kutokana na mzozo ‘ulioko’ ndani ya Simba.
Siku chache baada ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hii, Simba haikuwa ikipata matokeo ya kuridhisha kiasi cha kutafuta mchawi. Uongozi ukawasimamisha wachezaji wake kadhaa kwa madai ya kuhujumu timu.
Wachezaji waliosimamishwa ni Haruna Moshi ‘Boban’, Felix Sunzu, Amir Maftah, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Paul Ngalema, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ na Abdallah Juma. Lakini baadaye Kazimoto na Sunzu walisamehewa na kurejeshwa kundini.
Baada ya kuwasimamisha wachezaji hao ikaanza kuwatumia vijana kama Haruna Chanongo, Christopher Edward, Abdallah Seseme, Ramadhan Singano ‘Messi’, William Lucian, Miraji Adam, Hassan Khatib na Jonas Mkude.

TAZAMA KINACHOITWA KIKOSI CHA WATOTO
Hivyo kikosi cha sasa cha Simba mara nyingi hujumuisha wachezaji; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa, Messi, Felix Sunzu, Mkude na Haruna Chanongo.
Mashabiki wa Yanga wanabeza wanakiita kikosi hicho cha watoto, hivyo wanajipa imani timu yao inaweza kuinuka na ushindi wa mabao mengi wakiwa na ndoto ya kurudisha mabao 5-0 waliyofungwa katika mechi kama hii mwaka jana.
Uchambuzi unaonyesha Simba haina watoto. Katika kikosi hicho kinachoitwa cha watoto, unaweza kuona wachezaji watatu tu chipukizi au wasio na majina makubwa ambao ni Messi, Mkude na Chanongo.
Wachezaji wanane waliobaki ambao ni Kaseja, Chollo, Shamte, Kapombe, Mudde, Kiemba, Ngassa na Sunzu, wote ni wazoefu na wanaoweza kubadili matokeo wakati wowote ule. Mbali ya wachezaji hao, Simba ina Kazimoto ambaye yuko kikosini japokuwa tangu arudishwe amecheza mechi chache.
Hata hao chipukizi watatu ambao kuna uwezekano mkubwa wakawepo kikosi cha kwanza cha Simba,  ni wazoefu kwani wapo katika kikosi hicho kwa msimu wa pili sasa. Kikosi hicho kinaweza kutoka sare na Yanga au hata kushinda.
Wachezaji wanaoweza kuihofia Yanga ni chipukizi ambao msimu huu wanaichezea kikosi cha kwanza cha Simba kwa mara ya kwanza wakiwemo Lucian, Miraji na Khatib ambao hata hivyo kuna uhakika mdogo mno wa wao kuwemo kikosi cha kwanza.

YANGA WAKIJIAMINI, WAMEISHA
Wakati Yanga wataingia uwanjani wakijiamini, Simba kwa upande wao wataingia dimbani kufanya mambo mawili; kwanza kuthibitisha uwezo wao, pili kuwatibulia Yanga ili washerehekee kukabidhiwa kombe na kichapo juu.
Tatizo kubwa la kikosi cha Simba kwa sasa linaweza kuwa ni saikolojia kwa wachezaji baada ya kukosa hata nafasi ya tatu; pia kutoelewana miongoni mwao. Hata kufanya vibaya kwa Simba katika mechi za kwanza za mzunguko huu, kulisababishwa zaidi na uongozi.
Simba ilifanya vibaya katika mechi zake za Kanda ya Ziwa, kwani ilikubali kipigo cha bao 1-0 na Kagera Sugar kisha  ikatoka sare ya mabao 2-2 na Toto African ya Mwanza. Huo ulikuwa wakati ambao baadhi ya wanachama wa timu hiyo walikuwa wakipambana kumtoa madarakani Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage.
Katika mzozo huo Makamu mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ akajiuzulu. Mwingine aliyejiuzulu ni mjumbe wa kamati ya utendaji na mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hanspope, lakini sasa amerudi kundini.
Ghafla ‘watoto’ wa Simba chini ya Mfaransa, Patrick Liewig wakaanza kutoa darasa, wakailambisha JKT Mgambo 3-1, huku Yanga ikitoka sare na Coastal Union katika mchezo wake wa mwisho kabla ya kuivaa Simba keshokutwa.
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts na benchi lote la ufundi la Yanga, wanapaswa kutoruhusu mawazo ya mashabiki na baadhi ya viongozi wanaoibeza Simba.
MAKALA HII IMECHOTWA KATIKA GAZETI LA MAWIO IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI

TANZANIA YAJIONDOA MICHUANO YA COSAFA BAADA YA RATIBA KUINGILIANA NA CHAN

Tanzania (Taifa Stars) imejitoa kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika nchini Zambia kuanzia Julai 2-26 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah amesema Stars ambayo iliingizwa katika michuano hiyo kama timu mwalikwa imejitoa kutokana na mwingiliano wa ratiba kati ya michuano hiyo na mechi za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Amesema awali Tanzania ilithibitisha kushiriki michuano kwa matarajio kwamba Uganda ingekubali ombi la TFF la kubadilisha ratiba ya mechi za CHAN, lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) likagoma kwa vile kipindi ambacho kilipendekezwa lenyewe litakuwa na uchaguzi wa viongozi wao.

Taifa Stars itacheza na Uganda (The Cranes) katika mechi za CHAN ambapo mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu wakati ya marudiano itafanyika jijini Kampala kati ya Julai 26-28 mwaka huu.

Akizungumzia michuano ya COSAFA, Kocha Kim amesema angependa kushiriki michuano hiyo kwani ingekuwa kipimo kizuri kwa kikosi chake, lakini kwa sasa malengo makubwa ya Stars kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo fainali zake zitafanyika mwaka 2015.

HARUNA CHANONGO WA SIMBA, ZAHORO PAZI WAITWA TIMU YA TAIFA VS MOROCCO

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.

Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.

Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.

Kikosi kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;

Makipa ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Mudathiri Yahya (Azam) na Salum Abubakar (Azam).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu).

Kocha Kim amesema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24 ambapo Samata na Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini wachezaji atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo ataacha kipa mmoja na mchezaji mmoja wa ndani.

Awali TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu dhidi ya Algeria, Libya au Misri. Lakini baadaye Algeria ikasema itacheza na Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini Cairo, jambo ambalo lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya mashindano Juni 8 mwaka huu.

Kwa upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2 mwaka huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini Tripoli ambapo TFF ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.

CLOUDS THE DREAM TEAM KESHO KUKIPIGA NA IFM UWANJA WA NYUMBANI TANGANYIKA PARKERS

The Dream team ya Clouds FM kesho itadondoka kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Tanganyika Parkers kukipiga na timu ya chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM kuanzia majira ya saa 10 jioni.

SIKU KAMA YA LEO MWAKA 2012: PATRICK MAFISANGO ALIPOTEZA MAISHA YAKE KWA AJALI YA GARI



HILI NDIO GOLI LA MWISHO KUFUNGWA NA MAFISANGO WAKATI WA UHAI WAKE


Tarehe kama ya leo mwezi wa tano mwaka 2012, klanu ya ya Simba ilimpoteza kiungo wao wa kutumainiwa Patrick Mafisango Mutesa aliyepata ajali ya gari maeneo ya Tazara wakati akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na kwa bahati mbaya gari lake likakosa balance na kuingia mtaroni na hapo ndipo alipopeteza maisha.

Wednesday, May 15, 2013

CHELSEA WAWEKA HISTORIA YA KUBEBA UEFA CHAMPIONS LEAGUE NA EUROPA LEAGUE MFULULIZO


Benfica 1 Vs 2 Chelsea Final Europa League 15... by f100000904719795

MAALUM KWA MASHABIKI WA MAN UNITED: KAMPENI YA KUICHANGIA MAN UNITED FEDHA ZA KUMRUDISHA CRISTIANO RONALDO YAANZISHWA


Baada ya kuwa na wiki mbaya ya kuwaaga wapendwa wao kwenye klabu yao Sir Alex Ferguson na Paul Scholes, washabiki wa Manchester United wanaweza wakawa wanamkaribisha kipenzi chao Cristiano Ronaldo - ikiwa wao wenyewe wataweza kupata fedha za kumrudisha kutoka Real Madrid.

Kundi la mashabiki wa klabu hiyo kutoka Australia wametengeneza mtandao ambao mashabiki wa United wataweza kuchangia fedha za kuweza kumnunua mchezaji huyo kutoka Real Madrid, Ronaldo ana kiengele ambacho kimemuwekea thamani ya paundi millioni 100 kwa timu yoyote inayomtaka.

Harakati za mtandao wa 'BringRonaldoHome' zimeanza kuzaa matunda baada ya mashabiki maelfu kutuma maombi ya kununua jezi yenye jina la Ronaldo - lakini ili kampeni kufanikiwa inatakiwa wachangiaji millioni 10 watoa kiasi cha £10 kila mmoja ili kutimiza lengo.

Kwa kuwa United wanaripotiwa kuwa na mashabiki mil. 659 duniani kote, kufikisha £100 litakuwa jambo rahisi. 

Kampeni hiyo ya kumrudisha Ronaldo OT imezinduliwa siku 3 zilizopita, huku video kibao za mashabiki wa United wakihamasishana zikifurika kwenye mitandao ya facebook na Twitter. 

Fedha zitakazopatikana kupitia mtandao huo zitapelekwa kwa United kwa masharti - kuwawezesha kutumia fedha hizo za mchango wa mashabiki kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid. 

Ikiwa United watafanikiwa kumrudisha Ronaldo basi fedha zote zilizopatikana kupitia mtandao huo basi mashabiki wote waliochangia watatumiwa jezi zenye jina la Ronaldo - na ikiwa itashindikana kumrudisha CR7 Old Trafford basi kila aliyechangia atarudishiwa fedha zake. 
Mashabiki wanaweza kuchangia kupitia  www.bringronaldohome.org/

KITABU CHA MWAKALEBELA KUUZWA KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI

Na Mwandishi Wetu
KITABU cha kwanza nchini kinachozungumzia soka la Tanzania kijulikanacho kwa jina la “Soka la Tanzania” kitaanza kuuzwa siku ya mechi ya watani wa Jadi, Yanga na Simba iliyopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa.
Akizungumza na jijini jana, mtunzi wa kitabu hicho, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na yamedhaminiwa  na kampuni TSN Group kupitia kinywaji chake cha kuongeza nguvu Chilly Willy, Events World, Vannedrick Tanzania Limited na  Inbox Pub.
Wadhamini wengine ni Clouds FM, Times FM na Street Soul kwa mujibu wa Mwakalebela. Alisema kuwa kwa sasa ametoa nakala 10,000 kwa ajili ya kuuzwa Tanzania nzima. Alisema kuwa kitabu hicho kimezungumzia historia ya soka la Tanzania katika Nyanja za vijana, wanawake na wanaume, ligi kuu ya Tanzania Bara, Taifa Cup, Timu ya Taifa na Utawala Bora.
Mbali ya hayo, kitabu hicho kimezungumzia ujio wa kocha Marcio Maximo, mchango wa serikali katika kuinua mpira wa miguu, wadhamini, uhusiano kati ya waandishi wa habari na TFF na changamoto mbali mbali za mpira wa miguu Tanzania.
“Pia nimeelezea mambo niliyojifunza chini ya Rais Leodegar Tenga kwa kipindi cha miaka mine nikiwa TFF, matatizo niliyokutana nayo kutoka kwa makamandoo na kuniita mimi muimba kwaya wakati wa utambulisho wangu wa kwanza  Juni 15, 2006,” alisema Mwakalebela.
Alisema kuwa kitabu hichi ni muhimu sana kwa wana-habari, wachezaji, makocha, waamuzi na wadau wengine wa mchezo huo kwani kuna kumbukumbu zote za mechi za timu ya Taifa ikiwa mabao ya kufunga, wafungaji, vikosi tofauti vya timu za taifa na mambo mengine.

EUROPA LEAGUE FINAL: CHELSEA VS BENFICA - THE BLUES KUWEKA REKODI YA KUBEBA CHAMPIONS LEAGUE NA EUROPA LEAGUE MFULULIZO

Haijawa kutokea timu kuchukua ubingwa wa UEFA Champions League kisha kuchukua Europa League mfululizo, lakini hii ni rekodi ambayo Chelsea anaweza wakaiweka leo hii watakapocheza fainali ya Europa League na Benfica jijini Amsterdam Uholanzi. Katika kuelekea kwenye fainali hiyo tuangalie mambo muhimu kuhusu timu hizi mbili.

SAFARI YA TIMU ZOTE MPAKA KUFIKA FAINALI

Benfica
Ilishinda 1-0 vs Bayer Leverkusen
Ilishinda 2-1 vs Bayern Leverkusen
Ilishinda 1-0 vs  Bordeaux
Ilishinda 3-2 vs Bordeaux
Ilishinda 3-1 vs  Newcastle
Sare 1-1 vs Newcastle
Lost 1-0 vs Fenerbahce
Won 3-1 vs Fenerbahce

Chelsea
Ilishinda 1-0 vs Sparta Prague
Sare 1-1 @Stamford Bridge vs Sparta Prague
Walifungwa 1-0 vs Steaua Bucharest
Wakashinda 3-1 @Stamford Bridge Steaua Bucharest
Walishinda 3-1 Rubin Kazan
Wakafungwa 3-2 @Stamford Bridge vs Rubin Kazan
Walishinda 2-1 vs Basel
Wakashinda 3-1 @Stamford Bridge vs Basel
  
 

TAARIFA ZA TIMU

Benfica manager Jorge Jesus ana majeruhi mpya kwenye timu kuelekea fainali ya leo, ingawa mlinzi wa kulia Maxi Pereira amesimamishwa kwa kuwa na kadi za njano nyingi na hatocheza mchezo wa leo.
Chelsea boss Rafael Benitez tayari ameshathibitisha Eden Hazard hatocheza mechi ya leo na pia kuna wasiwasi kuhusu hatma ya John Terry.


BENFICA ITASHINDA IKIWA

Benfica wamefunga mabao 14 kwenye hatua za mtoano za Europa League, mabao sita yamefungwa na Oscar Cardozo.
Mparaguay huyo atakuwa miwba mchungu ikiwa atakuwa anapokea mipira mizuri kutoka kwa viungo wake, ingawa pia kuna hatari nyingine kwa Chelsea kutoka kwa Gaitan, Lima na Eduardo Salvio.
Katika safu ya ulinzi Benfica itabidi wacheze vizuri zaidi kuliko ilivyokuwa kwa Basel katika kuweza kuzuzia mashambulizi ya Chelsea - yenye watu hatari wanaoelewana kama Oscar, Juan Mata na Moses atakayechukua nafasi ya Hazard.

Fernando Torres anaweza kawa ndio mfungaji bora wa Chelsea kwenye michuano hii, lakini tishio la  Moses, Oscar na Juan Mata ambao watacheza nyuma yake ndio wakaisumbua sana safu ya ulinzi ya Benfica - na ikiwa Benfica wataweza kucheza vizuri dhidi watatu hao basi watakuwa wamejirahisishia kazi kwenye mchezo huo.

 CHELSEA ITASHINDA IKIWA
Inaonekana kama Chelsea wameweza kufika mpaka fainali lakini jasho haliwakuvuja la kutosha.
Ndio, kuna wakati walipata shida (hasa dhidi ya Rubin Kazan), lakini bado hawakuonekana kujali sana kuhusu kombe hili. na njia pekee ya kuweza kuwashinda Benfica walio kwenye bora kabisa itabidi wavuje jasho kweli kweli na kuweka umakini wao vizuri kwenye mechi ya leo.

Hazard, hatocheza leo, hivyo Mosses ambaye hutumia nguvu zaidi atachukua nafasi yake. Huku David Luiz akitarajiwa kucheza kwenye kiungo, hivyo The Blues watakuwa wapo vizuri kwenye ulinzi kiasi.

Wakati viungo wa Chelsea wanaokuwa kwenye kiwango chao, ni vigumu sana kushindana nao, ingawa mara nyingi inakuwa tatizo wanapocheza mabeki wa ulinzi imara na wenye kuelewana kama Luisao na Ezequiel Garay.
Gary Cahill na Branislav Ivanovic pia watakuwa na kazi ya kuhakikisha kijana wa kiparaguay na hatari Oscar Cardozo hakutani uso kwa uso na Peter Cech na kuwadhuru - Cordozo na hatari kwenye mipira hivyo itabidi wasimame nae kama wamegandanishwa nae na gundi.

 VIKOSI VINAVYOTARAJIWA

Benfica XI: Artur; Almeida, Garay, Luisao, Melgarejo; Matic, Perez; Salvio, Lima, Gaitan; Cardozo

 Chelsea XI: Cech; Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole; Ramires, David Luiz; Oscar, Mata, Moses; Torres

MSIMU MPYA WA THE LEGEND IS BACK!

Msimu mpya wa the legend is back , unaokwenda kwa jina la NIGHT OF THE LEGENDS au USIKU WA MALENGEDARI unaofanyika kila jumamosi katika ukumbi mpya ISUMBA LOUNGE zamani jollys club, wadau wote hasa wapenda burudani na mashabiki wa JOHN DILLINGA mnakaribishwa.

Tuesday, May 14, 2013

MABAO YA MCHEZO KATI YA AZAM FC NA MGAMBO JKT

HATIMAYE ARSENAL WAISHUSHA DARAJA WIGAN ATHLETIC - YAWA TIMU YA KWANZA KUSHINDA FA CUP NA KUSHUKA DARAJA


Arsenal vs Wigan 4:1 GOALS HIGHLIGHTS by footballdaily1

WATOTO WA MJINI ASHANTI UTD WAZINDUA TAWI JIPYA!

HAROUN CHANONGO IS ON FIRE!

KIBONZO CHA LEO!


MAHOJIANO NA MTANZANIA MOHAMMED KASSAM ALIYESHUHUDIA SEND OFF PARTY YA SIR ALEX FERGUSON.

SIMBA VS YANGA JUMAMOSI: HIVI NDIO VIINGILIO NA MWAMUZI ATAKAYEAMUA MCHEZO HUO

Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 18 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio hicho kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.

Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 30,000.  

Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni.

Mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro ambapo atasaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha, na Jesse Erasmo kutoka Morogoro. Mwamuzi wa akiba ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.

Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Leslie Liunda.

HATIMAYE TFF WATOA UFAFANUZI KUHUSU LIGI YA MABINGWA MIKOA

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) ilianza tarehe 12 Mei 2013 ikishirikisha klabu bingwa za mikoa yote ya Tanzania Bara, isipokuwa mikoa ya Pwani na Manyara ambayo kutokana na sababu tofauti ilishindwa kuwasilisha majina ya klabu zake hadi siku ya mwisho iliyowekwa na Kamati ya Mashindano, yaani tarehe 10 Mei 2013.

Suala la kukosekana kwa wawakilishi wa mikoa hiyo miwili limezua maswali mengi kiasi kwamba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linalazimika kutoa ufafanuzi kwa faida ya wadau wote wa mpira wa miguu.

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa, ambayo ni mpya baada ya TFF kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa mpira wa miguu, ilipangwa kuanza tarehe 5 Mei 2013, lakini hadi tarehe ya mwisho ya kuwasilisha majina ya mabingwa wa mikoa, yaani tarehe 2 Mei 2013 mikoa michache ndiyo iliyokuwa imemaliza ligi zao na kupata mabingwa.

Kuchelewa huko kwa mikoa kumaliza ligi zao kuliilazimisha Kamati ya Mashindano ya TFF kuongeza muda wa mikoa kuwasilisha majina ya wawakilishi hao hadi tarehe 10 Mei 2013 na hivyo siku ya kuanza kwa Ligi kusogezwa mbele hadi tarehe 12 Mei 2013.

Hadi kufikia tarehe hiyo mpya ya mwisho ya kuwasilisha majina ya mabingwa wa mikoa, ni mikoa sita tu iliyofaidika na kuongezwa huko kwa muda na kupata wawakilishi wake. Mikoa hiyo ni Iringa, ambayo pamoja na kuongezwa kwa muda, iliandika barua ya kuihakikishia Kamati ya Mashindano kuwa itapata bingwa kabla ya kuisha kwa siku ya tarehe 10 Mei 2013.

Mikoa mingine ni Lindi, Mtwara, Geita, Tabora na Dodoma.
Mkoa wa Manyara haukuweza kumaliza ligi yake hadi mwisho wa siku ya tarehe 10 Mei 2013 na hivyo Kamati ya Mashindano iliyosubiri majina hadi saa 12:00 jioni siku hiyo kuamua kuwaondoa wawakilishi wa Manyara kwenye ratiba.

Awali, Kamati ya Mashindano iliamua kuwa ratiba ya mechi za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa ipangwe tarehe 7 Mei 2013, ikishirikisha mikoa ambayo ilishapata mabingwa wake, lakini baada ya kuona baadhi ya mikoa ilikuwa haijakamilisha ligi zake, Kamati iliamua kuwa ratiba ipangwe kwa kutumia majina ya mikoa kwa matumaini kuwa hadi kufikia tarehe 10 Mei 2013, mikoa itakuwa imeshapata wawakilishi wake na kwa kuwa ratiba inahusu mikoa jirani, ingekuwa rahisi kwa timu kusafiri kutoka kituo kimoja hadi kingine.

Lakini Mkoa wa Manyara haukuweza kufanya hivyo na Kamati kulazimika kuuondoa kwenye ratiba kutokana na kushindwa kukidhi utashi huo.
Mkoa mwingine ambao uliondolewa kwenye ratiba ni Pwani ambayo pamoja na kutuma jina la mwakilishi wake, Kamati ilipokea malalamiko kutoka klabu zilizoshiriki Ligi ya Mkoa, zikidai kuwa jina la bingwa wa Pwani lililowasilishwa TFF lilikuwa batili kwa kuwa klabu ya Kiluvia United haikustahili kushiriki Ligi ya Mkoa kutokana na ukweli kuwa haijasajiliwa mkoani Pwani na wala haikushiriki ligi ya mkoa msimu uliopita. Kamati ya Mashindano iliiondoa Pwani kwenye ratiba na kulirudisha suala hilo mkoani.

Ingawa Katibu wa Pwani alijaribu kuishawishi Sekretarieti ya TFF iliangalie suala hilo kwa undani zaidi, Sekretarieti ilimjibu kuwa lilishafanyiwa uamuzi na Kamati, hivyo uamuzi huo usingeweza kutenguliwa na kumshauri katibu huyo arejee mkoani kwake kuwasiliana na viongozi wenzake kuona ni jinsi gani mkoa unaweza kunusuru hali hiyo kwa kufanya uamuzi ambao ungeuwezesha mkoa kupata mwakilishi.

Kwa mantiki hiyo, masuala ya Manyara na Pwani yalikuwa ndani ya uongozi wa mikoa husika na si Kamati ya Mashindano ya TFF kwa kuwa Kamati ilitaka ipatiwe jina la bingwa ambaye alipatikana kwa mujibu wa mfumo mpya wa Ligi ya Mikoa.

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na hivyo timu zilizokutana tarehe 12 Mei 2013, zitarudiana mwishoni mwa wiki hii na kupatikana timu zitakazosonga mbele kwenye raundi nyingine hadi timu tatu bora zitakazopanda daraja kwenda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zitakapopatikana.

Ligi za Mikoa, kwa mujibu wa kanuni mpya, zinatakiwa ziwe na timu kati ya 16 na 20 na zinatakiwa zicheze mechi mbili za nyumbani na ugenini, hata kama zitakuwa zinatumia uwanja mmoja.

Uamuzi wa kubadilisha mfumo huo ulifanywa ili kuhakikisha kuwa mikoa inakuwa na na mashindano kwa mwaka mzima na hivyo kuiwezesha mikoa kujikita katika kutafuta mbinu za kupata fedha na kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu kwenye mikoa yao.

Uamuzi huo pia unasaidia kupunguza mtindo wa wachezaji kuzunguka klabu tofauti katika msimu mmoja kwa kuwa wanalazimika kutulia kwenye klabu moja hadi muda wa usajili unapofika.

Pamoja na wachezaji kutulia sehemu moja kwa muda mrefu, pia walimu wanapata fursa ya kujikita vizuri kwenye programu zao kwa kuwa wanakuwa na uwezo wa kufuatilia maendeleo ya wachezaji wao.
Pamoja na hayo yote, mfumo huo utasaidia kurudisha msisimko kwenye mikoa na hivyo kutoa fursa kwa vijana wengi wenye vipaji kuonekana na kuendelezwa.

TFF inatoa wito kwa viongozi wa mikoa kuanza kubuni sasa mikakati ya kuendesha ligi hizo msimu unaokuja kwa kuwa hakutakuwa na nafasi tena ya kuongeza mud

KUONDOKA KWA WAYNE ROONEY OLD TRAFFORD NI BORA KWAKE NA MANCHESTER UNITED

  Kwenye mchezo wa mwisho wa kihistoria wa Alex Ferguson mbele ya mashabiki zaidi ya 70000 ndani ya  Old Trafford aliamua kumcheza Paul Scholes na kumuacha Wayne Rooney katika timu yake ya siku hiyo. Alisema kwamba alihisi akili ya Rooney ilikuwa sehemu nyingine baada ya mara nyingine kuomba kuondoka Old Trafford. Ferguson alisema amekataa ombi hilo na anaamini Rooney anahitaji muda tu kufikiria kwa kina kuhusu uamuzi wake, lakini naamini Rooney ni tatizo ambalo kocha mpya hahitaji.

Wayne Rooney alikuwepo uwanjani huku akicheka na kufurahia na wenzie kwa kuimba nyimbo za ushindi. Alionekana kuwa na furaha kabisa. Ulikuwa ni ushangiliaji ule ule ambao aliokuwa nao siku walipothibitisha ubingwa wao kwa kuwafunga Aston Villa alipokimbia na kwenda kumdandia mabegani Van Persie. Huyu hakuwa mchezaji ambaye hakuwa na furaha na mwenye kutaka kuhama, kwa hakika usingeona kama alikuwa na tatizo lolote. Lakini huwezi kuwajaji wacheza soka kwa ushangiliaji wao uwanjani bali ni uchezaji wao na ukweli ni kwamba katika miezi kadhaa iliyopita kiwango cha Wayne Rooney kimeonyesha kwamba mchezaji huyo hana furaha na maisha yake ndani ya Man United.

Wakati Rooney alipoibuka kwenye ulimwengu wa soka alionekana kuwa na kila kitu cha kuwa mchezaji wa daraja la juu kabisa duniani. Kwenye Euro 2004 alionekana kuwa na kasi, mwenye njaa ya mafanikio na adui mkubwa wa nyavu za wapinzani. Uhamisho wa kwenda United ulionekana sahihi kabisa - sehemu nzuri zaidi ya kukuza kipaji chake, lakini ikiwa karibia muongo mmoja umepita unaona kwamba Rooney hajafikia kule alipotakiwa kuwa. Kipaji ambacho kilitoa ahadi kubwa kimekosa msimamo imara.

Je Ferguson ameharibu kipaji?

Unaweza kumlaumu Alex Ferguson kwa kufeli kwa Rooney kuwa mchezaji wa daraja la juu kabisa duniani. Cristiano Ronaldo alichaguliwa kuwa mtoto wa kipekee ndani ya United wakati wawili hao wakiwa chipukizi na Rooney akawa mlishaji wa Ron kuliko kuwa mchezaji ambaye timu inamzunguka. Ndio Rooney alikuwa bora, lakini bado Ronaldo alipewa uhuru wa kuwa mchezaji muhimu wa timu na kujijenga kuwa mchezaji bora kabisa. Rooney akawa Robin kwa Batman. 

Je Ferguson angeweza kujenga timu kwa kumzunguka Rooney na kumsaidia kumjenga kuwa bora kabisa kama alivyotegemea baada ya Euro 2004? Inawezekana kabisa. Lakini Ferguson ni mtu ambaye anaangalia zaidi timu kuliko mchezaji binafsi na imani yake ilimtuma kwamba mafanikio ya timu yangekuja kwa kumfanya Ronaldo kuwa mchezaji muhimu wa timu. Ni vigumu kubisha ukiangalia namna United walivyopata mafanikio Ronaldo alipokuwepo  kama mchezaji anayecheza akiwa huru kwa timu kumzunguka yeye.
Sina mashaka kabisa kwamba kiwango cha Rooney kiliathiriwa na kucheza kwenye kivuli cha Ronaldo kwa muda mrefu na akakosa kuwemo katika ile miaka ya kujiendeleza ambayo ni wachezaji wachache wanapata. Hivyo si sawa kujaribu kwa sasa kumfananisha na wachezaji aina ya Messi na Cristiano. Pia Rooney amekuwa akitumika kama 'kiraka' na hilo nalo likamdumaza chini ya Ferguson.

Sio wachezaji wengi ambao wanaweza kuwa na ubora wa Rooney - kuweza kucheza popote pale mwalimu wao anapowataka kufanya hivyo, lakini hilo bado halikuweza kumfanya kuwa mchezaji wa daraja la juu kabisa duniani.

Kuomba kwako uhamisho

Mwaka 2010 wakati alipoongea hadharani kuhusu timu kukosa hamu ya mafanikio kwa kutosajili wachezaji wa daraja la juu, aliiweka United kwenye hali ya utata. Mwaka mmoja baada ya kuwapoteza Tevez na Ronaldo na kuwaleta wabadala Owen na Valencia ilikuwa wazi kabisa United walishuka kiubora. Ni kweli alichosema Rooney kuhusu timu yake lakini pia jambo hilo lilikuwa kinyume kabisa na utamaduni wa United.

Unaweza ukafikiria namna maoni yale ya Rooney yalivyomkasirisha Ferguson na kibaya zaidi hakuwa na namna zaidi ya kufanya liwezekanlo na kumbakisha mchezaji wake tegemeo kuliko kumpoteza kwa Man City - ingekuwa ni tukio baya sana  kwa United na mashabiki wake. Rooney akabakia United, na akishinda vita yake dhidi Fergie aliyejifanya mdogo na kumuomba Wayne abaki na tofauti na sera yake ya kuwafukuza wachezaji mastaa waliojiona wakubwa kuliko timu kama akina Beckham, Keane na Stam. Tangu wakati huo Rooney amekuwa sehemu ya timu japokuwa sio tegemeo kama ilivyokuwa huku nyuma.

Kwa matatizo yote ambayo yameonekana kuwepo baina ya Fergie United wameweza kubeba kombe lao msimu huu. Kwa kifupi msimu huu imeonekana wazi United hamhitaji Rooney kuweza kucheza vizuri. Usajili wa Robin van Persie na Shinji Kagawa ulileta maswali ya haraka haraka. "Ni wapi Rooney atacheza?" na ingawa Ferguson amefanya kazi nzuri katika kubadilisha kikosi chake ni wazi kwamba Van Perise ndio kiongozi wa mashambulizi ya timu na Kagawa na Welbeck wapo tayari kucheza kama wasaidizi wake.

Mechi dhidi ya Madrid zilionyesha wazi; Ferguson aliamua kumtumia Kagawa kwenye mechi ya kwanza na Welbeck katika mechi ya pili, Rooney alionekana kuwa angefaa zaidi kucheza kwenye jukumu la kuilinda timu katika mchezo wa pili. Fundisho lilonekana dhahiri, ikiwa utamkera Ferguson usidhani atasahau. Msimu wa 2010-11 Ferguson alimhitaji Rooney, lakini David Moyes ndani ya mwaka 2013 hamhitaji.

Rooney hahitajiki tena

Ferguson amemuachia Moyes timu nzuri sana yenye mchanganyiko mzuri wa wachezaji wenye uzoefu na wanaochipukia kuwa wanasoka wenye vipaji vya hali ya juu. Kagawa atakuwa bora zaidi msimu ujao na kama akifikia ule uwezo aliokuwa na Dortmund basi mashabiki wa United wategemee makubwa zaidi.

Ndio Moyes ataweza kupata changamoto za kuondokana na uzoefu ndani ya timu katika miaka inayofuatia; Scholes sasa ameondoka, Giggs, Ferdinand, Evra na hata Vidic wanaweza wakafuata nyayo za Paul Scholes misimu ijayo lakini bado kuna wachezaji chipukizi ndani ya Old Trafford ambao wanaonekana kuwa hatma nzuri ndani ya timu.

Swali kwa Moyes, je Moyes na United wanamhitaji Rooney? Ferguson amesema kwamba Rooney mwenye uwezo wa 100% angecheza kila dakika lakini bado siwezi kuacha kufikiria kwamba ooney hatoweza kufia uwezo wake kwa 100% akiwa ndani ya United na Ferguson anajua hili. Uhusiano wake na klabu kwa ujumla wakiwemo mashabiki umefikia pabaya. Maombi mawili ya kutaka kuondoka ndani ya miaka mitatu inaonyesha hali hali ilivyo.

Angeweza kuendelea kukaa na kuwa gwiji wa klabu ilivyo kwa akina Scholes au Giggs, au  pia angeweza kuvunja rekodi hata ya Bobby Charlton ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu na kujitengenezea ufalme ndani ya klabu kubwa kabisa duniani. Lakini uweledi mdogo wa Rooney ambao hauvumiliki ndani ya klabu ya aina ya United utamuondoa ndani ya klabu hiyo. Ameshapewa nafasi nyingi za kuwa mchezaji mwenye uelwedi ambaye United wanahitaji lakini ameshindwa. Hali ilivyo sasa kidogo inafanana na ilivyokuwa miaka ya mwisho ya David Beckham ndani ya Old Trafford.

United ni kubwa kuliko mchezaji yoyote na Ferguson ameonyesha hilo miaka yote akiwatimua bila huruma wachezaji kama Ince, Keane, Stam, Beckham na Van Nistelrooy. United waliendelea kupata mafanikio wakati wachezaji wakiwa hawapo na hakuna mashaka kwamba United wataendelea kufanya vizuri bila Rooney.

Ni bora zaidi kama ataondoka Old Trafford wakati huu. Moyes atataka kuja kwenye klabu bila kuwepo kwa msongamano wa habari na tetesi zinamhusu mchezaji mmoja kuliko timu yake kwa ujumla. Moyes anahitaji kumwambia Rooney hatoweza kumpa Rooney nafasi anayoitaka ndani ya timu. Kiukweli mfumo wa Van Persie/Kagawa unatoa ishara nzuri zaidi kwa mafanikio ya timu huku Welbeck na Hernandez wakitafuata muda zaidi wa kucheza, Rooney kubaki kutafanya mambo yazidi kuwa magumu kwa Moyes.

Ni muda wa kukiri kwamba muda wa Rooney ndani ya United umefikia mwisho. Tena inawezekana amekaa kwa muda mrefu zaidi ilivyotakiwa. Lakini kabla ya msimu huu United wamekuwa wakimhitaji zaidi Rooney lakini sasa umuhimu huo umepungua. Hii inanikumbusha sakata la Ronaldinho na Barcelona mwaka 2008, alikuwa na misimu miwili ya nyuma ambayo alianza kupoteza fomu yake na ubora na Guardiola alijua kwamba ili kuendelea mbele ingebidi mbrazili huyo aondoke. Ni vigumu kuacha kuona ufanano wa suala hili la Rooney na Ronaldinho. 

Wapi ataenda? United hawatomuuza kwa timu ya kiingereza, Man United sio Arsenal. Na kuwa mkweli kabisa ada ya uhamisho wa Rooney na mshahara wake unaweza ukaziondoa timu nyingi kwenye mbio za kumsaini ndio maana sitoshangazwa kumuona akijiunga aidha Madrid au PSG msimu ujao.

Nilisemaga msimu uliopita Rooney anahitaji kuondoka United kwa maendeleo yake binafsi kama mchezaji kwa kuwa mmoja ya wachezaji watatu wa kiwango cha juu duniani. Ingeweza kuwa uamuzi mzuri ambao angeweza kuufanya, pia uamuzi huo ungemsaidia yeye kukua kama mchezaji na kuisadia timu yake ya taifa ya England.

United watatengeneza fedha nzuri kwa biashara ya Rooney na kuondokana na mzigo wa kulipa zaidi ya £200,000 ya mshahara. Ni jambo zuri kwa pande zote. Wote wamesaidiana na kufanikiwa katika maisha yao ya pamoja lakini bado ilivyo kwa mahusiano mengine inabidi ujue wakati wa kuachana.

WEWE UNAMKUMBUKA KWA KIPI RONALDO LUIS NAZARIO DE LIMA!


Mimi ninachokikumbuka juu ya huyu jamaa,wakati alipojiunga na Inter Milan ya Italia akitokea FC Barcelona aliikuta jezi namba 9 ya Inter inavaliwa na mshambuliaji raia wa Chile Ivan Zamorano "BamBam " kwaiyo akapewa jezi ambayo binafsi naipenda kupita maelezo,jezi namba 10 lakini kwa kuwa kulikuwa na kipengele kwenye mkataba wake kilichokuwa kinailazimu Inter kumpatia jezi namba 9 msimu ulifuata ilibidi Zamorano anyang'anywe jezi yake nambari 9 ili apewe Ronaldo.

Kwasababu Zamorano pia alikuwa  ni muumini wa jezi ya namba 9 ili aweze kuendelea kuivaa ilimbidi ile namba 18 aliyopewa aifanyie udambwiudambwi kwa kuweka alama ya kujumlisha katikati ya moja na nane lengo likiwa ni kuipata namba yake ile ile tisa.! Huyu jamaa alikua mbunifu kila mahala. JE WEWE UNAMKUMBUKA DE LIMA KWA KIPI ?

PICHA YA SIKU: SIKU SHAFFIH DAUDA ALIPOGOMA KUMWAGIWA POMBE NA WACHEZAJI WA BAYERN MUNICH!

 Kwenye picha kutoka kushoto: Phillip Lahm,Jerome Boateng,Mario Gomez,Shaffih Dauda,Arjen Robben,Toni Kroos na Thomas Muller

Monday, May 13, 2013

BREAKING NEWS: ROBERTO MANCINI ATIMULIWA KUIFUNDISHA MANCHESTER CITY - MSAIDIZI WAKE KUBEBA JAHAZI MPAKA MWISHO MWA MSIMU


Roberto Mancini of Manchester City
Tetesi zilianza kusambaa kuhusu hatma ya kocha wa Manchester City Roberto Mancini hata kabla ya mchezo wa fainali wa FA Cup.
Lakini muda mfupi uliopita kocha huyo wa kitaliano amefukuzwa rasmi kazi ya kuifundisha Manchester City huku Manuel Pellegrini, kocha wa Málaga, akitajwa kuwa yupo mbioni kuchukua nafasi ya muitaliano huyo. 

Hatma ya Mancini ilianza kuonekana kwenye mashaka kufuatiwa kuibuka kwa taarifa huko Spain usiku wa kuamkia siku ya fainali ya FA Cup ambapo City walifungwa na Wigan na siku iliyofuata ilionekana wazi kwamba wamiliki wa timu hiyo kutoka Abu Dhabi wamepoteza imani na kocha huyo. 

Mancini ndio kocha aliyewapa City ubingwa wao wa kwanza tangu mwaka 1968, ametimuliwa baada ya timu yake kukosa kikombe hata kimoja msimu huu huku akifanya vibaya katika michuano ya ulaya 
 
Mwenyekiti wa City Khaldoon Al Mubarakalisema: "Rekodi ya Roberto inaongea yenyewe, amekuwa na wakati mzuri hapa na ameweza kupata mapenzi ya mshabiki na heshima pia.
"Amefanya kazi nzuri na kutuletea makombe.
"Tunamtakia mafanikio mema siku za mbele na tunamshukuru kwa yote aliyotufanyia."

Kocha msaidizi Brian Kidd atachukua nafasi ya Mancini mpaka mwishoni mwa msimu - akimalizia mechi mbili zilizobakia za premier league.

BAADA YA KUMWAGIWA POMBE - FRANCK RIBERY AAPA KUTOONGEA TENA NA JEROME BOATENG

Franck Ribery ameapa kutoongea tena na mchezaji mwenzie wa Bayern Munich Jerome Boateng baada ya kulowanishwa kwa pombe wakati wa wakishangilia ubingwa wa Bundesliga wikiendi iliyopita.

Mfaransa huyo ambaye ni muislamu wa swala tano - alijaribu kukimbia ili aepuke ushangiliaji wa kumwagiana pombe wa wachezaji wenzie baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo walioshinda  3-0 dhidi ya Augsburg.
Lakini pamoja na kujaribu sana kukwepa kuguswa na pombe - ambayo ni haramu kwa dini yake - Ribery hatimaye aliogeshwa na na Boateng.

Akiwa amekasirishwa kabisa kwa kitendo hicho cha mjerumani, winga huyo alisema: ‘Sitoongea tena na Boateng, anajua mie muislam. Nimeudhiwa sana na kitendo chake.’
Mlinzi David Alaba na kiungo Anatoliy Tymoshchuk pia walijiunga na Boateng kumlowesha Ribery, ambaye alionekana kutulia kwa wakati huo.
Golikipa Manuel Neuer kwa busara kabisa yeye alijiepusha na suala hilo na kuamua kuwamwagia baadhi ya mashabiki walionekana kupendezewa na ushangiliaji huyo.

PSG WATHIBITISHA REAL MADRID WAMEPELEKA OFA YA KUMTAKA ANCELOTTI - LAKINI WAMEWAKATALIA

Paris St Germain imekataa ofa ya Real Madrid kutaka kumsaini kocha wao Carlo Ancelotti, raisi w klabu hiyo  Nasser al Khelaifi amesema leo Jumatatu.
"Wao (Real) walikuja na tukajadili suala. Carlo ana mkataba na sisi kwa mwaka mmoja zaidi..... kwangu mimi naamini atakuwa hapa msimu ujao," Al Khelaifi aliiambia Reuters.
"Ni mtu mzuri sana na nina uhakika atauheshimu mkataba wake."
Ancelotti amekataa kuthibitisha kwamba ataendela kubaki PSG jana Jumapili wakati waliposhinda kombe lao la kwanza tangu la Ligue 1 tangu msimu 1994.
"Tutaongea na klabu kuhusu suala hili," alisema muitaliano huyo ambaye alijiunga na klabu hiyo December 2011.
Al Khelaifi alielezea kwamba hana haraka yoyote ya kujadili suala hilo na Ancelotti ambaye amekuwa akihusishwa na kujiunga na Real katika wiki kadhaa zilizopita baada ya vyombo vya habari kusema kwamba Jose Mourinho ataondoka kwenye klabu hiyo ya Spain na kurudi kwenye timu yake ya zamani ya Chelsea.
"Kwa sasa sina mpango wowote wa kukutana nae kwa sababu ana mkataba na klabu. Sasa ni muda wa kusherehekea ubingwa" alisema raisi wa PSG.
Al Khelaifi pia aliongeza anataka kuongeza urefu wa mkataba wa David Beckham baada ya nahodha huyo wa zamani wa England kujiunga na klabu hiyo mwezi January.
"David ni mchezaji wa aina yake, mweledi na mtu mzuri sana. Tunataka kuendelea kuwa nae hapa lakini inategemea na atakachoamua mwenyewe," alisema.
"Ana furaha kuwa hapa, niliongea nae jana na wiki iliyopita na ameonyesha kwamba anaweza akabaki."

KATUNI YA LEO!