Search This Blog

Loading...

Saturday, July 9, 2011

COUNTDOWN SIMBA VS YANGA :BINGWA ATAAMULIWA NA MATUTA..

Hatimaye matarajio ya watanzania wengi yametimia kwani michuano ya Kagame Castle Cup inafikia tamati kwa mchezo wa fainali unaowakutanisha wenyeji Simba na Yanga . Kama ungemuuliza shabiki yoyote wa vilabu hivi nani angetwaa uchampioni wa michuano hii mwanzoni ni dhahiri angekwambia kuwa timu yake itashinda hivyo njia pekee ya kumaliza ubishi huu ilikuwa kukutana kwenye mchezo wa fainali anayeshinda ashinde na anayefungwa angoje siku nyingine .
Ukitazama timu hizi mbili kila moja ina sehemu yake ambayo inaipa kiburi na uhakika wa kuibuka ushindi lakini upande wa pili nao kila timu ina mapungufu yake ambayo yanaipa woga .

Besena na Falsafa ya ulinzi..
Makocha wa timu hizi mbili kidogo wamekuja na falsafa tofauti hasa kwa kocha wa Simba Moses Basena . Mganda huyu ameifanya Simba iwe na safu ya ulinzi ambayo ina uimara ambao ulikosekana msimu uliopita wa ligi ya Vodacom . Labda hii ni kwa sababu timu hii imekosa wamaliziaji huku ikiwa na viungo wengi ambao wanapenda kuuchezea mpira hali inayoweza kuwagharimu wanapokutana na timu inayolinda kwa nidhamu ya hali ya juu na ndio maana hadi michuano hii inafikia hatua ya fainali Simba imeruhusu wavu wake kuguswa mara mbili tu . Hivyo nadhani ni sahihi kusema kuwa Basena ana falsafa ambayo inazingatia zaidi ulinzi.

Sam Timbe Kuimalisha kiungo…
Kwa upande wa Jangwani mganda mwingine Sam Timbe anaonekana kuwa mtu ambaye anapenda timu yake ishambulie mwanzo mwisho huku ikiwatumia walinzi wanaotumia nguvu sana wakati wanapokabiliana na washambuliaji toka timu pinzani , labda ni kwa sababu ya aina ya uchezaji wa walinzi alio nao ambao ni watu “physical” kina Fusso,Cannavaro,Taita na Oscar Joshua. Timbe anaonekana kuwa ameibadilisha Yanga kwa kiasi kikubwa kwenye safu ya kiungo ambayo inaongozwa na Rashidi Gumbo mchezaji aliyesajiliwa toka Simba akishirikiana na kiungo mwingine Nurdin Bakari ambaye naye alitoka Simba muda mrefu kidogo uliopita .Watu hawa wameonekana sana kuelewana kwenye safu ya kiungo tofauti na ilivyo falsafa halisi ya Yanga ambayo kihistoria hupenda kuwatumia zaidi mawinga kama kina Ngassa, Nsa Job , Edibily Lunyamila na wengine wengi waliopita siku za nyuma japo hawajaitupilia mbali falsafa hii kwani wapo Julius Mrope na Kiggi Makasi . Safu ya Ushambuliaji ya Yanga ndio inayoonekana kuwa na uhai zaidi unapopambanua safu mbili za ushambuliaji za Simba na Yanga . Hadi kufikia fainali Yanga imetupia wavunia mabao saba kwenye hatua ya makundi na kwenye mechi za mtoano walishindwa kufunga bao hata moja na kupita kwa njia ya matuta. Simba wao wamefunga mabao sita hadi kufikia hatua hii.
Simba kutokua na mshambuliaji asilia…
Ukitazama vikosi vya timu zote mbili Yanga wanaonekana kuwa kamili kuliko Simba kwani wanaonekana kuwa na “first eleven” inayoeleweka na ambayo inaweza kujenga “chemistry” yaani maelewano tofauti na Simba ambao kikosi chao sio kile kile na kimekuwa kikibadilika badilika sana karibu kila mechi . Unaweza kukuta leo Banka anacheza nafasi ya namba tisa , kesho akacheza kumi na mwenendo ndio umekuwa huo karibu kila mechi .
Hili linaweza kuwa na hasara au faida kwa sababu wakati mwingine mpinzani anaweza kukosa mbinu ya kukabili kwa sababu tu ameshindwa kujua ni timu ipi itakayoingia siku hiyo na hasara yake ni pale ambapo timu yako haina “chemistry” kitu ambacho Yanga wanaonekana kuwa nacho .Simba tangu mchezo wa kwanza dhidi ya Vital O wamegharimiwa na tatizo moja kubwa ambalo ni kukosa wamaliziaji , hili limesababisha wekundu kukosa mabao mengi sana ya wazi . Ukitazama mfumo ambao wanaingia nao ambao huwa unabadilika badilika hata mchezoni Simba wamekuwa wakiwatumia mabeki wane , viungo wanne na washambuliaji (viungo wanaolazimika kucheza kama washambuliaji) wawili wanaocheza mmoja mbele mmoja nyuma katika mfumo wa 4-4-1-1 na wakati mwingine wanacheza 4-4-2 diamond huku kiungo mmoja akisimama mbela ya mabeki na mwingine nyuma ya washambuliaji na hata wakati mwingine wamekuwa wakicheza 4-1-3-2 au 4-1-3-1-1 ambapo mara nyingi unakuta kaseja anasimama langoni chollo akisimama kulia , amir maftah akisimama kushoto na wawili kati ya Waluhya Derick,Kevin Yondani na Juma Nyoso wakisimama kati na kuna wakati Derick waluhya alisimama pembeni kulia jambo ambalo almanusra liwaletee Simba balaa na kwenye safu ya kiungo Jerry Santo amekuwa akisimama kama namba sita kwenye nafasi ya holding au combat midfielder akiwa mchezaji pekee kwenye safu hiyo aliyecheza kwa “consistency” ya hali ya juu huku pembeni kulia akicheza wakati mwingine Salum Machaku na wakati mwingine Ulimboka na Musa Hassan Mgosi amekuwa akicheza kama kiungo anayetokea upande wa kushoto na Shija Mkina amekuwa akiingia tokea benchi la wachezaji wa akiba kujaza nafasi ya winga ya kulia . Safu ya viungo wa Simba imejaa watu ambao wanajua kuuchezaea mpira kwa ufundi wa hali ya juu na wanapiga pasi nyingi sana nzuri ila shida kubwa imekuwa kwenye umaliziaji ambako Mohamed Banka na Haruna Moshi wamekuwa wakipangwa kama washambuliaji. Watu hawa wawili kiasili ni viungo ambao wanacheza namba nane au kama wakicheza ushambuliaji wanacheza namba kumi nyuma ya mshambuliaji .Sasa wanapocheza kama washambuliaji Simba inakosa mabao mengi sana kwa kuwa hawa watu si wafungaji ufundi wao wote unaishia kwenye pasi za mwisho na sio kuzipasia nyavu .




Mfumo wa Yanga ni 4:4:2 na 4:4:1:1
Kwa upande wa Yanga wamekuwa wakitumia mfumo wa 4-4-2 au 4-4-1-1 yaani mabeki wakiwa kwenye mstari mmoja , viungo kwenye mstari mmoja na washambuliaji wawili moja nyuma ya mwingine . Godfrey Taita,Shadrack Nsajigwa , Oscar Joshua , Chacha Marwa na Nadir Haroub Canavaro wamekuwa wakisimama kwenye mstari wa walinzi wa Yanga na kati ya hawa Chacha Marwa ameonekana kuwa “outstanding ” kuliko wenzie kwa jinsi anavyocheza kwa ujasiri akikabiliana na washambuliaji kwenye zile “one-to-one situation” . Kwa walinzi wa Yanga shida imekuwa moja nayo ni kutumia nguvu nyingi kuliko maarifa na wakati mwingine wanapokutana na washambuliaji wanaocheza ‘begani’ mwa beki wamekuwa wakichanganyikiwa kama ilivyotokea kwa Jonas Sakuwaha wa AL Mareikh na Owen Kasule wa Bunamwaya ambapo mara zote hizo Yanga walijikuta wakiruhusu mabao ya kizembe . Viungo wa yanga wamekuwa wakicheza vyema , Nurdin Bakari amekuwa aki-link vyema na Rashid Gumbo na Julius Mrope kwa upande wake amekuwa akiwapa wakati mgumu sana mabeki kwa kasi yake na chenga , Kiggi Makasi yeye ameonekana kuwa na homa za vipindi kwani kuna wakati anakuwa hayuko mcchezoni ana anakuwa anaipa timu yake wakati mgumu kwani inakuwa kama inacheza pungufu japo mipira yake anayoileta toka upande wa kushoto ina madhara sana .
Washambuliaji wa Yanga ndio wamekuwa gumzo haswa Hamis Kiiza na Davis Mwape japo jinsi wanavyotumiwa kidogo inatia mashaka . Davis Mwape amekuwa akilazimika kucheza nyuma ya mshambuliaji mwingine jambo ambalo kwa mwili wake mkubwa linamshinda kwa sababu anashindwa kupima dribbling zake , kuna wakati ambapo anashindwa kupiga mahesabu ya wakati gani wa kuusogeza mpira na wakati gani wa kuupiga , kama angekuwa kiungo hili lisingempa shida ila kwa kuwa yeye ni aina ya wachezaji tunaowaita “18 yard players” yaani mchezaji wa kwenye eneo la 18 tu na nje ya hapo si mahala kwake . Pamoja na hayo ameweza kufunga mabao mawili ambapo mojawapo alilofunga dhidi ya Bunamwaya lilikuwa bao muhimu kwani liipa Yanga ushindi ambao uliwahakikishia uongozi wa kundi . Hamis Kiiza kwa upande wake ameonyesha umahiri wake kwenye ufungaji na kama Simba hawatampa ulinzi wa kutosha hakika atawaliza .
Kukosekana kwa Boban na Santo

Tatizo moja ambalo Simba watakuwa nalo kwenye mchezo wa fainali dhidi ya watani wao ni kuwakosa Haruna Moshi na Jerry Santo ambao wana kadi mbili zilizofuatana . Wote walipata kadi za njano kwenye mechi ya Robo fainali dhidi ya Bunamwaya na wakapata teka kadi kama hiyo dhidi ya Al Mareikh kwenye nusu . Kati ya hawa Simba watamkosa sana Jerry Santo mtu ambaye ukimuacha Juma Kaseja kama Simba wakitwaa ubingwa huu basi anaweza kuwa mchezaji wao wa michuano . Santo ni mtu anayetambua majukumu yake na anayatimiza kwa asilimia zote . Kukosekana kwa Boban kunaweza kusiwe pengo kubwa kwa sababu wapo watu ambao wanaweza kujaza nafasi yake vyema . Kumkosa Santo kunaweza kumaanisha kuwa Basena akalazimika kumtumia mtu kama Waluhya kama jeraha lake litapona katika nafasi ya kiungo wa chini au Patrick Mafisango japo Mafisango ni mzuri sana kwa kiungo cha juu .Kwa upande wa Kevin Yondani na Juma Nyoso watakuwepo japo Derick Waluhya kama atapona atakuwa na umuhimu wake kwa jinsi alivyo na uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo kuwaliko wenzie anaopigania nao nafasi ya beki wa kati, Ulimboka mwakingwe ameonyesha kiwangi kizuri katika mechi zake zote alizocheza na uzoefu wake wa mechi kama hii unampa faida ya ziada ya kupewa nafasi . Kama kanuni ziotaruhusu na kama Simba walisajili mapema jina la Mwinyi kazimoto na kama atapangwa atakuwa na umuhimu kwa jinsi anavyojua jukumu la “playmaker” na anaweza kuwa na mchango mkubwa sana.
Yanga na kikosi kamili..
Yanga wanaingia wakiwa na kikosi kizima ambacho hakina mapungufu yoyote . Golini akiwepo Yaw Berko ambaye ukiacha kungushwa na mabeki wake ni “reliable” sana golini , Nsajigwa , Taita , Canavarro na Chacha Marwa ni watu ambao wameonyesha uwezo wakiwa kwenye nafasi ya Ulinzi na hakuna sababu ya kutowapanga kwenye fainali , Gumbo na Nurdin moja kwa moja wana nafasi zao kwenye kikosi cha kwanza kama ilivyo kwa maforward wawili Mwape na Kiiza japo rekodi inaweza kumfanya Timbe alazimike kumtumia Jerryson Tegete kwani amekuwa akiwafunga Simba mara kwa mara na uwepo wake uwanjani unawafanya walinzi wa Simba na kipa wao kuwa roho juu.
Sam Timbe
vs Moses Basena..
Makocha wa timu zote mbili wana historian a Michuano hii . Sam Timbe amewahi kutwaa ubingwa mara tatu akiwa na timu tatu tofauti . Labda historia itampendelea tena na kumpa ubingwa wan ne na wa kihistoria . Bassena amewahi kucheza fainali mara moja ambapo alipoteza kwa Tusker Fc iliyokuwa inaongozwa na nahodha Jerry Santo katika mwaka ambao Yanga ilimkimbia mnyama kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu . je ataendelea na historia yake ya kuwasindikiza wenzie ?
Ukitazama historia ya vilabu hivi viwili kwenye michuano hii unapata sababu ya ziada ya kununua tiketi mapema na kuwahi kuingia uwanjani . Timu hizi zimewahi kukutana mara mbili ambapo kila mmoja ameshinda mara moja na atakeyeshinda safari hii atakuwa mbele ya mwenzie .
Itakuwa fainali ngumu sana kwa sababu timu hizi zina historia ambayo iko mbali zaidi ya michuano hii na kwa kila mmoja kumfunga mwenzie kwa njia yoyote ile ni jambo la thamani kubwa sana na mchezo huu unaongezewa utamu na ukweli kuwa ni mchezo wa fainali ambao lazima mshindi apatikane. Je itakuwa kijani na njano au nyekundu na nyeupe ambao wataitawala Afrika mashariki na kati? Jibu litapatikana baada ya dakika tisini au 120 au baada ya mikwaju ya penati iwe mitano au ile ya piga ni kupige hadi mtu afe .

prediction:Mshindi atapatiana baada ya dakika 90.

COUNTDOWN KAGAME CASTLE CUP FINAL: SIMBA vs YANGA.


MASHABIKI wa soka nchini hawakuwa na imani kabisa na timu zao, Simba na Yanga kama zinaweza kufika hata Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Castle, kutokana na sababu tatu kubwa, ambazo ni; kukurupushwa kuingia kwenye michunao hiyo, maandalizi duni na pia kushuka kwa viwango vya timu zetu katika miaka ya karibuni.
Lakini hali imekuwa tofauti, miamba hiyo ya soka ya Tanzania miaka nenda, rudi leo inakutana kwenye fainali ya michuano hiyo, baada ya kufanya kazi ngumu kuanzia mechi za makundi hadi Robo Fainali na Nusu Fainali.
Simba iliyokuwa Kundi A, ilifuzu kama kinara wa kundi hilo, baada ya kujikusanyia pointi nane kutokana kushinda mechi mbili na kutoka sare mbili, utamu zaidi kipa Juma Kaseja akiweka rekodi ya kuwa mlinda mlango pekee ambaye hakuruhusu nyavu zake kutikiswa hata mara moja katika hatua ya makundi.
Simba ikakutana na mabingwa wa Uganda, Bunamwaya FC katika Robo Fainali na wakafanikiwa kushinda mabao 2-1, shukrani kwake kiungo Mkenya, Jerry Santo Evans aliyefunga bao la ushindi dakika ya 84, katika mchezo ambao dhahiri ulikuwa mgumu kwa Wekundu wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Simba ikakutana na timu ngumu, tena sana kulingana na timu zote zilizokuwa kwenye michuano hii, El Merreikh ya Sudan, wengi miongoni mwa wachambuzi wa soka wakiipa timu hiyo kura chache mno za kukata tiketi ya kucheza mechi ya mwisho.
Mchezo ulianza vibaya kwa Simba, wakitanguliwa kufungwa bao na mabingwa wa Sudan, dakika ya 12 mfungaji akiwa ni Adiko Rime, kabla ya mshambuliaji mkongwe Ulimboka Alfred Mwakingwe kuisawazishia timu hiyo bao tamu kwa kichwa cha mkizi, dakika ya 24.
Dakika 90 zilitimu matokeo yakiwa 1-1 na dakika 30 za nyongeza pia hazikubadilisha matokeo na ndipo mchezo ulipohamia kwenye mikwaju ya penalti, Simba ikashinda 6-5, shujaa wa michomo hiyo Juma Kaseja akicheza penalti ya Mzambia Jonas Sakuwaha.
Sasa Simba leo watamenyana na watani wao wa jadi, Yanga katika fainali, hii ikiwa ni mara ya tatu kihistoria timu hiyo kukutana katika hatua hiyo ya michuano hii, kwanza mwaka 1975 na pili mwaka 1992, mechi zote zikipigwa visiwani Zanzibar na kila timu ilishinda mechi moja.
Mabao ya Sunday Manara na Gibson Sembuli (sasa marehemu) mwaka 1975 yaliipa Yanga ushindi wa 2-0 dhidi ya Simba waliokuwa mabingwa watetezi na kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza- wakati ushujaa wa kipa Mwameja Mohamed kupangua mikwaju ya penalti uliipa Simba ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa tena taji hilo.
Kwa Dar es Salaam Simba na Yanga hazijawahi kukutana kwenye michuano ya Kagame, ingawa mwaka 2008 zilipaswa kumenyana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu, lakini Watoto wa Jangwani ‘wakapotea’ njia ya kuelekea ulipo Uwanja wa Taifa, na Wekundu wa Msimbazi wakapewa ushindi wa mezani.

SIMBA ILIVYOTWAA MATAJI SITA YA AWALI:
Simba ndio bingwa wa kihistoria wa michuano hii, ikiwa imetwaa taji hilo mara sita, ikifuatiwa na AFC Leopards na Tusker za Kenya, ambazo zote zimetwaa taji hilo mara tano kila moja, wakati Yanga sawa na APR FC ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, SC Villa ya Uganda zimetwaa mara tatu kila moja taji hilo.
Luo Union, El-Merreikh zimechukua mara mbili kila moja, ATRACO, Rayon Sport za Rwanda, KCC na Polisi FC za Uganda kila moja imetwaa mara moja.

ZANZIBAR MWAKA 2002:
Michuano ya mwaka huo, ilianza Februari 16, ikishirikisha timu za Prince Louis ya Burundi, Mebrat Hail ya Ethiopia, Oserian Fastac, Tusker FC za Kenya, waliokuwa mabingwa watetezi, APR ya Rwanda, Elman ya Somalia, Simba SC, SC Villa na wenyeji Forodha na Mlandege za Zanzibar.
Simba ilipangwa Kundi B pamoja na Tusker, Forodha, Prince Louis na Elman na mechi ya kwanza Februari 8, ililazimishwa sare ya bila kufungana na Elman, kabla ya Februari 21 kutoka nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Seleman Nsabah dakika ya 14 na kuifunga 2-1 Prince Louis, Emmanuel Gabriel akisawazisha dakika ya 27 kabla ya Yussuf Macho ‘Musso’ kufunga la pili dakika ya 78.
Febaruari 23 katika mchezo wa tatu, Simba iliitandika Forodha mabao 3-1, Joseph Kaniki akitangulia kufunga dakika ya 22, Steven Mapunda ‘Garrincha’ akifunga la pili dakika ya 65 na Macho kupiga la tatu dakika ya 90 na Februari 25, Wekundu hao wa Msimbazi walihitimisha mechi zao za Kundi B kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya 1-0, waliojifunga wenyewe dakika ya 88, Kevin Malumbe akimfunga kipa wake katika harakati za kuokoa.
Kwa matokeo hayo, Simba iliongoza Kundi hilo kwa pointi zake 10, na kwenye Nusu Fainali Machi Mosi, iliifunga Mlandege mabao 2-0, wafungaji
Macho dakika ya 37 na Sheikhan Rashid kwa penalti dakika ya 90, kabla ya kuifunga Prince Louis Machi 3 kwenye fainali, bao pekee la Nteze John Lungu dakika ya suita ya mchezo.
Siku hiyo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Mohamed Mwameja, Said Sued, Ramadhani Wasso/ Majuto Komu dk 35, Amri Said, Boniface Pawasa, Suleiman Matola, Stephen Mapunda/Joseph Kaniki dk 74, Shekhan Rashid, Yusuf Macho, Nteze John/Emmanuel Gabriel dk 61 na Mark Sirengo.

DAR ES SALAAM MWAKA 1996:
Michuano ya mwaka huo, Simba ikiwa bingwa mtetezi ilipangwa Kundi A pamoja na Al Hilal ya Sudan, APR ya Rwanda na Small Simba ya Zanzibar.
Ilianza kwa kuifunga 2-0 Small Simba, kabla ya kufungwa 1-0 na APR na baadaye kuibwaga 1-0 Al Hilal.
Simba ikafuzu kuingia Nusu Fainali kama mshindi wa pili wa Kundi hilo,na kukutana na Gor Mahia ya Kenya na kufanikiwa kushinda 1-0, bao pekee la Bitta John.
Katika fainali, Simba ilikutana na APR na bao pekee la beki mahiri enzi hizo George Magere Masatu dakika ya 115, baada ya kutimu dakika 90 bila timu kufungana, liliipa Simba ubingwa wa tano wa michuano hiyo.

DAR ES SALAAM MWAKA 1995:
Michuano ya mwaka huo pia ilifanyika Dar es Salaam na Simba walipangwa Kundi A tena pamoja na Express ya Uganda, Morris Supplies ya Somalia na Adulis ya Somalia.
Katika mchezo wa kwanza ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Express, kabla ya kuifunga Morris Supplies 3-1 na Adulis 4-1, hivyo kuongoza Kundi hilo kwa kufikisha pointi saba na kutinga Nusu Fainali, ambako ilikutana na El Mourada ya Sudan Februari 9 na kushinda 1-0, hivyo kujikatia tiketi ya fainali.
Ilikutana na Express ya Uganda katika fainali na dakika 120 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, Hussein Amaan Marsha akitangulia kuwafungia waganda katika harakati za kuokoa dakika ya 51, lakini swahiba wake George Masatu akasawazisha dakika ya 53.
Dakika 120 zikamalizika timu hizo zikiwa zimefungana 1-1 na ndipo kwa mara nyingine, umahiri wa kipa Mwameja Mohamed ukainufaisha Simba kwenye mikwaju ya penalti na ikashinda 5-3.

ZANZIBAR MWAKA 1992:
Wakiwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, walikutana na watani wao wa jadi, Yanga katika fainali.
Kwa kuwa mwaka 1975 Yanga iliifunga Simba mabao 2-0 visiwani Zanzibar, wengi waliamini historia itajirudia na mwaka 1992, ila mambo yakawa tofauti.
Ikitokea Kundi A, Simba ilizipiga Bata Bullets ya Malawi na Small Simba ya Zanzibar na kutinga Nusu Fainali, ambako iliifunga Rivatex Eldoret ya Kenya mabao 2-0.
Katika fainali, dakika 120 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 na mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti na kwa mara nyingine kipa wa zamani wa Reading ya England, Mwameja Mohamed akaonyesha umahiri wake kwa kucheza penalti ya Abubakar Salum ‘Sure Boy’ na baadaye ya David Mwakalebela hivyo kuipa Simba ubingwa wa mwaka huo.

DAR ES SALAAM MWAKA 1991:
Kombe hilo halikuwahi kukanyaga tena Tanzania, tangu Yanga waende kuliacha Kenya mwaka 1976 na michuano ya mwaka 1991 ilikuwa mkombozi wa taifa letu.
Ikishirikisha timu za Gor Mahia ya Kenya, Limbe Leaf Wanderers ya Malawi,
El-Maorada ya Sudan, SC Villa ya Uganda na wenyeji Simba SC na Coastal Union ya Tanga, ilifanyika katika vituo vya Dar es Salaam na Tanga.
Simba iliongoza Kundi A mjini Dar es Salaam na kutinga Nusu Fainali ambako iliifunga Gor Mahia na kukata tiketi ya kuingia fainali ilipokutana na SC Villa ambako ilishinda mabao 3-0, wafungaji Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’ aliyefunga mawili na Hassan Afif moja.
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba kilichorejesha Kombe hilo nchini kilikuwa; Iddi Pazi, Raphael Paul, Twaha Hamidu, Jamhuri Kihwelo ‘Mrema’, Method Mogella (sasa marehemu), Iddi Suleiman ‘Meya’, Issa Kihange, Bakari Iddi, Ayoub Mzee/Hassan Afif, Zamoyoni Mogella na Itutu Kigi ‘Road Master’.
Ambao hawakushirikii mechi hiyo walikuwa ni Mackenzie Ramadhan, Khalfan Ngassa, Gebo Peter, Hasan Banda, Mavumbi Omar, Hamisi Gaga, Frank Kasanga Bwalya.
Mambo mawili ya kukumbukwa kwenye michuano hii; kipa Iddi Pazi ‘Father’ alicheza mechi zote za Simba bila kuruhusu bao hata moja, lakini pia kocha Abdallah Kibadeni ‘King’ alimfukuza beki tegemeo wa timu hiyo wakati huo Frank Kasanga ‘Bwalya’ kwa utovu wa nidhamu na akaamua kumtumia kama sentahafu kiungo Method Mogella badala ya kiungo.

DAR ES SALAAM MWAKA 1974:
Hii ilikuwa michuano ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kufanyika na ilichezwa kwa mtindo wa Ligi mjini Dar es Salaam ikishirikisha timu za Simba SC, Navy FC ya Zanzibar, Simba ya Uganda na Abaluhya FC ya Kenya.
Simba ilianza kwa sare ya 2-2 na Navy FC, kabla ya kuifunga Abaluhya FC 1-0 na badaaye kutoka sare ya bila kufungana na Polisi Uganda.
Kwa matokeo hayo, Simba ikachukua ubingwa kwa kufikisha pointi tano, ikifuatiwa na Abaluhya iliyofikisha pointi tatu, Navy pointi mbili sawa na Simba ya Uganda.
Hivyo ndivyo Simba ilivyotwaa mataji yake sita, vipi kwa watani wao wa jadi, Yanga walichukuaje mataji yao matatu?





YANGA ILIVYOTWAA MATAJI MATATU YA AWALI:
Yanga iliyokuwa Kundi B la michuano ya mwaka huu, ilifuzu kama kinara wa kundi baada ya kujikusanyia pointi saba kutokana na kushinda mechi mbili na kutoka sare moja.
Katika Robo Fainali, Yanga ilikutana na Red Sea ya Eritrea na kushinda kwa penalti 6-5, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo huo.
Katika Nusu Fainali, Yanga ilikutana na St George ya Ethiopia na kushinda tena kwa penalti 5-4, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120. Sasa leo inacheza fainali na watani wao wa jadi, Simba SC, hii ikiwa ni mara ya tatu kwao kukutana kwenye fainali ya michuano hiyo. Yanga tayari ina mataji ya michuano hiyo na leo inasaka la nne, je hayo matatu ilichukuaje?

ZANZIBAR MWAKA 1975:
Iliingia kama bingwa wa Tanzania baada ya kuifunga Simba SC katika fainali ya Ligi mwaka 1974 Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, wakati watani wao hao waliingia kama mabingwa watetezi wa michuano.
Yanga ilipangwa Kundi B pamoja na Express ya Uganda na Mufulira Wanderers ya Zambia. Yanga ilianza kwa kuifunga Express FC mabao 4-0 na baadaye kutoka sare ya 1-1 na Mufulira, hivyo kuongoza Kundi hilo na kukata tiketi ya kuingia Nusu Fainali.
Katika Nusu Fainali, Yanga iliifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 na kukata tiketi ya kuingia fainali Janauri 13, mwaka huo ilipokutana na watani wao wa jadi, Simba SC.
Mabao ya Sunday Manara ‘Computer’ na Sembuli yaliipa Yanga ushindi wa 2-0 na taji la kwanza la michuano hiyo.

KAMPALA, UGANDA MWAKA 1993:
Ilikwenda kama bingwa wa Bara na watano wao, Simba walikwenda kama watetezi wa taji na huko Yanga walipangwa Kundi A pamoja na wenyeji SC Villa na Malindi ya Zanzibar.
Katika mchezo wa kwanza, Yanga ilifungwa 3-1 na Villa, siku hiyo kabla ya kuibuka na kuifunga Malindi mabao 2-1, yote yakitiwa kimiani na Said Nassor Mwamba ‘Kizota’, sasa marehemu, hivyo kukata tiketi ya kuingia Nusu Fainali.
Katika Nusu Fainali, Yanga ilikutana na Express FC na kushinda mabao 3-1, hivyo kutinga fainali ambako ilikutana tena na SC Villa.
Kwa kuzingatia matokeo ya mchezo wa awali kwenye Kundi A, Yanga haikupewa nafasi kabisa ya kufurukuta mbele ya SC Villa, lakini mambo yalikuwa tofauti, mabao ya Said Mwamba na Edibily Lunyamila, yaliipa timu hiyo ushindi wa 2-1 pamoja na taji la pili la michuano hiyo.
Marehemu Kizota aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.

KAMPALA, UGANDA MWAKA 1999:
Ilikwenda kama bingwa wa Bara, ikiwa mwakilishi pekee na ilitua huko, huku mashabiki wengi wa soka Uganda wakiwa na kumbukumbu ya kile kilichofanywa na klabu hiyo mwaka 1993.
Timu zilizoshiriki michuano hiyo ni Vital'O ya Burundi, Mebrat Hail ya Ethiopia, AFC Leopards ya Kenya, Kiyovu Sport, Rayon Sport za Rwanda,
Naadiga Dekedaha ya Somalia, KMKM ya Zanzibar, Al Hilal ya Sudan, Yanga, wenyeji Express na SC Villa za Uganda wakati Red Sea ya Eritrea ilijitoa dakika za mwishoni.
Kwa matokeo hayo, Kundi D ilimokuwa Yanga lilibakiwa na timu mbili tu, yaani mabingwa hao wa Bara na mabingwa watetezi.
Mechi ya kwanza, Yanga ilifungwa 3-0 na Rayon Januari 4 na ziliporudiana siku mbili baadaye, Yanga walilipa kisasi kwa ushindi wa 3-0 pia, mabao ya
Sekilojo Chambua dakika ya 23 na 57 na Kali Ongala dakika ya 59.
Katika Robo Fanali, Yanga ilikutana na Al Hilal Januari 10 na kushinda mabao 2-1, wafungaji Salvatory Edward dakika ya 14 na Edibily Lunyamila dakika ya 89 kwa penalti.
Katika Nusu Fainali, Yanga ilikutana na Vital’O ya Burundi Januari 13 na kushinda mabao 3-2, wafungaji Kally Ongara dakika ya 16, Bakari Malima dakika ya 78 na Said Mhando dakika ya 90.
Hivyo kwa mara ya pili, Yanga ilikutana na SC Villa kwenye fainali kukumbushia vitu vya mwaka 1993 na safari hii mambo yalikuwa mazito zaidi, kwani dakika 120 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 Lunyamila akiisawazishia Yanga dakika ya 42, baada ya Hassan Mubiru kutangulia kufunga dakika ya saba tu ya mchezo huo.
Mchezo ukahamia kwenye mikwaju ya penalti na Manyika Pater akaingia kwenye orodha ya makipa hodari wa kupangua penalti baada ya kupangua mikwaju miwili, Yanga ikishinda kwa penalti 4-1, Uwanja wa Nakivubo.
Hivyo ndivyo Yanga ilivyotwaa mataji yake matatu na leo inashuka dimbani kuwania taji la nne, je mambo yatakuwaje? Hapana shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona mambo yatakuwaje Uwanja wa Taifa jioni ya leo.

COUNTDOWN TO KAGAME CASTLE CUP FINAL:VITUKO VYA MECHI ZA WATANI WAJADI


Timu mbili zenye upinzani wa enzi na enzi katika soka la Tanzania Yanga na Simba Jumapili hii july 10 zinakutana katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Kagame Castle cup mwaka 2011, mchezo huo utakaofanyika kwenye uwanja Mkuu wa Taifa jijini Dar es Salaam. Blog yako inaaangalia baadhi ya vituko vya kusisimua vilivyowahi kutokea wakati wa matayarisho, wakati au baada ya michezo baina ya timu mbili hizo kumalizika.
- Mwaka 1968 katika matayarisho ya mechi ya Simba (wakati huo Sunderland) na Yanga mchezaji wa Simba Emmnuel Mbele ‘Dubu’ alikuwa amefungiwa kucheza mpira kwa kipindi cha miezi 6 kutokana na utovu wa nidhamu uliotokea katika moja ya michezo ya ligi (wakati huo ligi ya taifa). Mchezo huo ulikuwa umepangwa kufanyika uwanja wa Ilala (Sasa Uwanja wa Karume zilipo ofisi za TFF). Timu zote mbili zilifika uwanjani huku wachezaji wakiwa tayari wamevaa jezi lakini kumbe Suderland hawakuwa tayari kucheza mchezo huo kwa madai kwa sharti kuwa wasingecheza huku mchezaji wao tegemeo, Mbele akiwa amefungiwa. Kutokana na hali hiyo kikaitishwa kikao cha dharura kilichohusisha viongozi wa Chama cha mpira wa Miguu Tanganyika (Tanganyika Football Assocation - TFA) Sunderland na Yanga. Baada ya hoja ya Sunderland kuwekwa mezani huku ikiaminika kuwa Yanga walikuwa wakihofia uwezo wa Mbele, Kwa mshangao Yanga waliwaambia viongozi wa TFA kuwa kama kikwazo cha mchezo ilikuwa ni mchezji mmoja tu basi afuguliwe na mchezo uendelee. TFA ikamfugulia Mbele ili akipige. Mchezo ukachezwa Sunderland wakapata kipigo cha aina yake cha magoli 5-0 yaliyofungwa na Maulid Diluga (2), Salehe Zimbwe (2) na Kitwana Manara.

- Agosti 10, 1974 Uwanja wa Nyamagana Mwanza magwiji wawili Gibson Sembuli (Yanga) na Saad Ally (Simba) waligongana katika harakati za kuwania mpira katika mchezo huo unaoaminika kuwa moja ya michezo iliyokuwa ya kiwango cha juu kabisa katika historia ya timu hizo mbili. Inaaaminika kuwa mahali walipogongana magwiji hao kiliota kichuguu ambacho hadi leo kipo. Bado hakuna uthibitisho wa kisayansi kuwa kichuguu hicho kilitokana na kugongana huko.

- Agosti 10, 1985 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam mlinzi wa kati wa Simba Twalib Hilal anaushika mbira uliokuwa ukilekea golini baada ya kupigwa kichwa na Abeid Mziba-aliyejipatia umaarufu mkubwa wa kufuga magoli kwa kichwa kuliko miguu. Inaamuliwa ipigwe adhabu kubwa (penati) kuelekea laqngo mwa mwa Simba. Mpira unawekwa na anakwenda kupiga Juma Mkambi ‘Jenerali’ Simba wanatoka katika eneo la mita kumi na nane ili penati ipigwe lakini ghafla mpigaji anabadilishwa na anakwenda kupiga Hussein Iddi. Kuona hivyo Zamoyoni Mogella (wa Simba) anakimbia na kuupiga nje ili penati isipigwe. Mpira unavunjika na baadaye Yanga wanapewa ushindi wa magoli 2-0 na kuibuka mabingwa mwaka huo.

- Agosti 31, 1991 Katika kile kilichoonesha imani za ushirikina zilizopindukia mipaka, ilinunuliwa mipira mipya ya kuchezea kwenye mchezo huo chini ya uwakilishi wa wazee wawili mmoja kutoka kila upande wa Simba na Yanga na kisha wazee hao wakaiweka mipira hiyo ndani ya mfuko mmoja na kwenda nayo uwanjani wakiilinda kwa zaidi ya saa nne hadi pambano lilipoanza. Simba ilipokea kipigo cha goli 1-0 lililofungwa na Said Sued ‘Scud’.

- Novemba 13, 1991, (Ligi ya Muungano), Mchezo wa marudiano wa ligi hiyo ulifikia mapumziko huku timu hizo zikiwa hazijafungama. Timu zilipoingia katika vyumba vya kubadilishia mavazi, Simba hawakurejea dimbani. Madai ambayo hadi leo hayajawahi kuthibitishwa na mtu au chombo chochote ni kuwa mwamuzi wa mchezo huo – Hafidh Ali alinukuliwa akiwaambia wachezaji wa Simba kuwa wangepokea kipigo cha magoli 3-0 iwapo wangethubutu kurejea uwanjani baada ya mapumziko.

- Septemba 26, 1992 Yanga iliyokuwa tayari imetawazwa mabingwa kwa mwaka wa pili mfululizo iligoma kupeleka timu uwanja wa Taifa kwa madai kuwa mchezo huo haukuwa na umuhimu wowote kwao, hivyo Simba ikapewa ushindi na chama cha mpira wa miguu FAT.




- Julai 2, 1994 Yanga inafungwa goli 4-1 kipigo ambacho kinabakia kuwa kikubwa zaidi cha karibuni katika michezo ya ligi. Magoli ya George Masatu, Atuman China, Madaraka Seleman na Dua Said yalitosha kuikandamiza Yanga huku goli la Yanga likifungwa na Costantine Kimanda. Baada ya mchezo ambao ulichangia kuipa Simba ubingwa baada ya kuukosa kwa miaka mitatu, timu ya Yanga ikisambaratika huku wachezaji waandamizi kama Stephene Nemes, Said Mwamba, Nico Bambaga na Edibily Lunyamila wakiiacha timu hiyo ikipepesuka na hatimaye kusajili wachezaji wengi vijana wakiwemo Willy Mtendamema, Nonda Shaban Maalim Saleh na Sylvatus Ibrahim ‘Polisi’

- Februari 25, 1996 Simba iligoma kupeleka timu uwanja wa Taifa ikiishinikiza FAT kuilipa kwanza fedha kutoka CAF kutokana na faini iliyolipwa na klabu ya Chapungu ya Zimbabwe. Chapungu ilitozwa faini hiyo baada ya kushindwa kusafiri nchini kucheza mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika. Inasadikiwa kuwa Simba haikuwahi kulipwa deni hilo.

- 2002, mchezo ambao ulikuwa umepangwa miezi kadhaa uliahirishwa dakika za mwisho kwa amri ya Waziri wa Kazi Maendeleo ya Vijana na michezo Juma Kapuya kutokana kile ambacho Yanga walidai walikuwa wakinyanyaswa kisaiklojia baada ya kiungo wao wa pembeni kulia Said Maulid ‘SMG’ kutangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa si raia wa Tanzania. Mchezo huo ulichezwa baadaye na timu hizo kutoka sare ya magoli 2-2.

- Oktoba 24, 2007 Uwanja wa Jamhuri Morogogoro; Pambano linamalizika huku Simba wakiwa washindi goli 1-0 la Ulimboka Mwakingwe. Baada ya hapo mashabiki wa Yanga wanawashmbulia baadhi ya wachezaji na kuwapiga wakati wakielekea kupanda gari lao. Jioni hiyohiyo baadhi ya wchezaji waliopigwa kipa Ivo Mapunda na mlinzi Shadrack Nsajigwa wanaondoka kambini wakidai kuhofia usalama wao. Uongozi wa Yanga unakutana siku chache baadaye na kuamua kuwafungia kutocheza mpira kwa kipindi cha miezi 6.

- Julai 27, 2008 (Kombe la Kagame). Yanga inakataa kupeleka timu uwanjani kuikabili Simba katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu ya Kombe la Kagame ambao ungekuwa mchezo wa kwanza kuzikutanisha timu hizo katika Uwanja Mkuu wa Taifa. Yanga ilidai kuwa haikupeleka timu kwa vile haikutekelezewa ahadi ya kulipwa na TFF shilingi milioni 50 kabla ya mchezo huo kama yalivyokuwa makubaliano ya kuwalipa Yanga na Simba kila moja kiasi hicho cha fedha. Yanga inaadhibiwa na CECAFA kutocheza michezo yake kwa kipindi cha miaka 3 na pia kutozwa faini ya Dola za Marekani 35,000. TFF nayo inaifungia Yanga kutocheza michezo yote ya kimataifa ya kirafiki na mashindano kwa kipindi cha miaka miwili. Hata hivyo adhabu hiyo ilitenguliwa baadaye na Kamati ya Nidhamu ya TFF na badala yake Yanga ikatozwa faini ya Dola za Marekani 20,000 na kutakiwa kuiomba radhi TFF na wadau wa mpira wote nchini.

NGASSA SAFARINI U.S KWA MILLIONI 12


Mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka nchini Tanzania Mrisho Khalfan Ngassa anayeitumikia klabu tajiri nchini Bongo Azam FC, anaondoka leo saa 3 usiku kuelekea Obamaland kwa ajili kufanya majaribio na klabu ya Seattle Sounders. Ngassa anatarajiwa kuondoka nchini na ndege ya shirika la Continental Airlines kwa tiketi ya Business class yenye thamani ya $7500. Ngassa akiwa U.S na Seattle katika majaribio atacheza katika mechi kati ya Seattle Sounders dhidi ya Manchester United itakayofanyika Julai 20 mwaka huu.
Now we can see that Ngassa is getting the treatments of a Football superstar.

COUNTDOWN KAGAME CASTLE CUP FINAL: SIMBA vs YANGA.


Pazia la michuano ya 37 ya kombe la Kagame kwa ngazi ya vilabu vya ukanda wa Afrika ya mashariki na kati, linafungwa hapo kesho kwenye uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam, kwa mchezo wa fainali utakaowakutanisha mafahari wawili wa soka la Bongo.

Ni Simba na Young Africans, pambano ambalo linajulikana kama Dar es salaam Derby, linalowakutanisha mahasimu wa kandanda wan chi ya Tanzania, kwa miaka dahar sasa.

Hii ni fainali yao ya tatu, kukutana kwenye michuano mikubwa katika ngazi ya vilabu vya ukanda huu wa Cecafa, baada ya kuwa zimlikwishafanya hivyo katika miaka ya 1975 na 1992 pale visiwani Zanzibar kwenye uwanja wa Aman.

Mwaka 1975, fainali hiyo ilizikutanisha timu hizo, na Young Africans ikaibuka mbabe kwa kuibwaga Simba mabao mawili kwa sifuri, katika fainali ya kusisimua ya michuano iliyokuwa ya pili.

Simba, mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, wakalipa kisasi kwenye uwanja huo huo wa Aman mnamo mwaka 1992, kwa ushindi wa changamoto ya mapigo ya penati, mitano kwa minne, kufuatia sare ya bao moja kwa moja mnamo dakika mia moja na ishirini za mchezo.

Katika ardhi ya Tanzania bara, bado wana wa Jangwani hawajaonja ladha ya kutwaa uchampioni huo, na hii ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukipiga kwenye mchezo wa fainali katika ardhi hii ya Tanzania bara, japo mara mbili zimekutana kwenye ardhi ya upande wa pili, wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Ni mchezo ambao unazikutanisha timu mbili zilizo na sura nyingi mpya, tofauti na ilivyozoeleka, kwani takriban nusu ya kila kikosi, kina wanandinga wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ya Premier ya Tanzania bara, na mashindano ya kimataifa.

Simba, bingwa wa kihistoria wa michuano hii, inaingia uwanja mkuu wa taifa hapo kesho ikisaka heshima zaidi kwenye michuano hii, kwani itakuwa inasaka ubingwa wake wa saba, baada ya kuwa ilikwishafanya hivyo mara sita.

Ina historia nzuri pale michuano hii inapofanyika kwenye uwanja wa nyumbani, na haijawahi kushindwa katika mchezo wa fainali ya michuano hii kwenye ardhi ya Tanzania bara.





Mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni mnamo mwaka 2002 pale kwenye uwanja wa Aman visiwani Zanzibar, ikiondosha St Louis ya Bujumbura Burundi kwa kuilaza bao moja kwa sifuri, hivyo ina kiu ya ubingwa huo kwa kipindi cha miaka nane.

Kwa upande wa mahasimu wao Dar es salaam Young Africans wameshindwa kuupata ubingwa huo tangia walipofanya hivyo mnamo mwaka 1999 kule mjini Kampala nchini Uganda, kwa kuilaza sports club Villa ya Uganda kwa changamoto ya mapigo ya penati, minne kwa mmoja.

Miamba hawa wa bara wamekuwa na historia nzuri ya kutwaa ubingwa huu nje ya ardhi ya Tanzania, kwani kabla ya mwaka huo wa 1999, ilifanya vivyo hivyo kwenye uwanja wa Nkivubo mjini Kampala kwa kuilaza pia Villa mabao mawili kwa moja.

Katika fainali kumi ilizocheza za michuano hiyo, Simba ilipoteza kwenye fainali dhidi ya Young Africans mnamo mwaka 1975 kule visiwani ZANZIBAR, ikapoteza kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Kampala City Council mitatu kwa miwili mnamo mwaka 1978, kisha ikapoteza mnamo mwaka 1981 kule jijini Nairobi nchini Kenya mbele ya Gor Mahia ikilala bao moja kwa sifuri na dhidi ya Villa mjini Kampala kwa kulala pia bao moja kwa sifuri lililowekwa kimiani na mshambuliaji Vincent Tendwa.

Young Africans imecheza fainali sita za michuano hii, ambapo ilipoteza kwenye fainali tatu, ikiwamo dhidi ya Luo Union ya Kenya mnamo mwaka 1976 kwa kulala mabao mawili kwa moja, kisha mnamo mwaka 1986 dhidi ya El Mereikh kwenye uwanja wa taifa wa zamani jijini Dar es salaam kwa changamoto ya mikwaju ya penati, minne kwa miwili baada ya sare ya mabao mawili kwa mawili kwenye dakika 120.

Kisha ikipoteza dhidi ya hasimu wake Simba kwa changamoto ya mikwaju ya penati mitano kwa minne kwenye uwanja wa Aman visiwani Zanzibar, mnamo mwaka 1992, baada ya sare ya bao moja kwa moja kwenye dakika 120 za mchezo.

EXCLUSIVE: MR.LIVERPOOL ACHUKUA NAFASI YA NDIMBO SIMBA.


Miezi michache baada ya kujiuzulu kwa Cliford Mario Ndimbo kujiuzulu nafasi ya usemaji ndani ya klabu ya Simba, klabu hiyo leo imemteua Ezekiel Kamwaga a.k.a Mr.Liverpool kuwa msemaji rasmi wa timu hiyo.
Ezekiel ambaye ni moja kati wanahabari wakongwe nchini anakuwa ni msemaji wa pili wa klabu hiyo ndani ya uongozi wa Simba chini ya Aden Rage.

Friday, July 8, 2011

EXCLUSIVE: MWINYI KAZIMOTO ASAJILIWA RASMI SIMBA

KAZIMOTO AKIWA RAISI KIKWETE-IKULU


Kiungo wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaitumikia klabu ya JKT Ruvu msimu uliopita Mwinyi Kazimoto amekamilisha rasmi taratibu za uhamisho wake wa kujiunga klabu bingwa ya kihistoria ya Cecafa Kagame Castle Cup-Simba Sports Club.

Kukamilika kwa usajili wa mchezaji huyu ambaye amekuwa kwenye rada za Msimbazi kwa takribani miaka miwili kunamaanisha mchezaji kwa sasa ana uhalali wa kuitumikia Simba kuanzia katika mechi ya Fainali ya Kagame Cup dhidi ya Yanga na kuendelea.

HEARTS OF OAK NA ASANTE KOTOKO WAOTA MBAWA


Mashindano yaliyokuwa yawashirikishe timu kongwe za barani la Afrika kutoka nchini Ghana, Hearts of Oak na Asante Kotoko kwa pamoja na 2011 Kagame Castle Cup’s finalists Simba na Yanga hayatakuwepo tena.

Mashindano hayo ambayo yalipewa jina la “Tanzania International Cup” na yalipangwa kufanyika ndani ya siku mbili kupitia usimamizi wa kampuni mbili za Afrika Kusini Lumuli Marketing na Octagon.

Chanzo cha kutofanyika kwa michuano kunasemekana ni waandaji kushindwa kuhimili gharama kubwa za kutumia uwanja wa taifa walizotajiwa na wasimamizi wa uwanja huo.

BREAKING NEWS: YANGA YAMSAJILI IDRISA RAJABU

Klabu Bingwa ya Tanzania Bara Dar Young African wamefanikiwa kumsajili mchezaji wa Sofapaka ya Kenya na timu ya taifa ya Tanzania Idrisa Rajabu.
Idrisa ambaye hucheza upande wa beki wa kushoto alisajiliwa Sofapaka akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro misimu miwili iliyopita, na sasa anarejea Tz kuja kuitumikia Yanga.

SHAY GIVEN KUHAMIA VILLA WIKI IJAYO


Aston Villa wana matumaini kuwa Shay Given atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Alex McLeish wiki ijayo kwa dili la paundi 3.5 million kutoka Manchester City.
Villa wanataka huduma za kipa huyo kutoka Ireland ambaye amekosa nafasi ndani ya kikosi cha Eastlands ili kumbadili golikipa Brad Friedel aliyehamia Tottenham.
Klabu hizo mbili kwa muda sasa wamekuwa kwenye mazungumzo na chanzo cha habari kutoka Villa zinasema dili hilo kumsajili kipa huyo litakamilika wiki ijayo.
Given alikuwa namba 1 akiwa Newcastle kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 kabla hajaamia City miaka miwili iliyopita.

WAYNE ROONEY AMVALISHA MWANAE JEZI EVERTON.

Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney leo ame-post picha ya mtoto wake wa kiume KAI akiwa amevaa jezi ya timu aliyokuwa anaichezea zamani ya Everton, huku akihaidi kutoa picha nyingine ya mtoto wake akiwa amevaa jezi mpya ya United, Kesho.

WANYAMA AKARIBIA KUTUA CELTICS


Mdogo wake kiungo wa kimataifa wa Kenya anayecheza soka lake huko Italia kwneye klabu ya Inter Milan McDonald Mariga anayekwenda kwa jina Victor Wanyama Mugabe yuko mbioni kujiunga na klabu kubwa nchini Scotland ya Glasgow Celtics . Wanyama ambaye ambaye ameichezea timu yake ya taifa ya Harambee Stars mara kadhaa na anakaribia kusaini kuichezea Celtics baada ya kushinda rufaa yake ya kibali cha kazi nchini Scotland. Wanyama ambaye ana umri wa miaka 20 alikuwa anaichezea Germinal Beerschot na anaongeza idadi ya Waafrika mashariki wanaocheza soka huko Scotland baada ya Mganda David Obua ambaye anaichezea Hearts baada ya kusajili toka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

LIVERPOOL KUWAFUATA ARSENAL NA MAN CITY


Baada ya Manchester City na Arsenal kuuza haki za jina uwanja wao, sasa klabu ya Liverpool nayo iko mbioni kuuhama uwanja wake wa kihistoria wa Anfield . Klabu hiyo kwa sasa iko mbioni kuanza mradi wa kujenga uwanja mwingine lakini ili kufanikisha mradi huo klabu hiyo inatakiwa kutengeneza fedha za ziada ambazo kwa taarifa toka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa italazimika kuuza haki za kuupa jina uwanja wa Anfield YAANI “Naming Rights ” kwa kampuni itakayofika bei na kutoa fedha ambazo zitatumika kujenga uwanja mwingine kama ilivyokuwa kwa uwanja wa Arsenal The Emirates ambao kampuni ya usafiri wa Anga inayomiliki ndege za Emirates ambayo inadhamini uwanja huo kwa kuwa imelipia haki za kutumia jina la Brand yao kama jina la uwanja . Sasa unapoingia kwenye uwanja wa Anfield kaka inavyoonekana hapo kwenye picha inayomuonyesha Fernando Torres na Rafa Benitez kuna bango limeandikwa “THIS IS ANFIELD”, je Bango hili litabailishwa na kuandikwa “THIS ISN’T ANFIELD”??

KUTOKA EASTLANDS MPAKA ETIHAD STADIUM NA £100M


MANCHESTER CITY wametangaza dili lilivunja rekodi kupitia udhamini wa Etihad Airways.
Matajiri wa Premier League wameuza haki za jina la uwanja wao wa Eastlands, ambao sasa utajulikana kama Etihad Stadium. The Abu Dhabi Airline wamekubali kutoa udhamini wa miaka 10 wenye thamani paundi millioni 100, hivyo kuushinda mkataba kati ya Arsenal na Emirates Airline ambao nao una thamani ya £ 100m lakini ukiwa ni kwa kipindi cha miaka 10 kwa ajili ya kuupa jina la "Emirates " uwanja wa Gunners. Manchester City's CEO Garry Cook ameusifu mkataba huo kuwa ndio bora na muhimu katika historia ya soka.
"Tuna furaha kutangaza kuongeza mkataba wetu na Etihad Airways.Partnership yetu haitakuwa kwa jezi pekee lakini pia utahusu uwanja wetu- Etihad Stadium.Sehemu pana inayozunguka uwanja itajulikana kama "Etihad Campus".Kuna vitu vingine kama vile media, biashara na ushirikiano wa jamii na vitu vingine vingi. "Pengine huu unaweza kuwa mkataba mzuri zaidi katika historia ya Soka." Etihad tayari wameshakuwa wadhamini wa jezi za City kwa mkataba wa £ 2.8m per year. Huu ni mfano mwingine wa uwekezaji mkubwa kutoka Abu Dhabi ndani ya klabu hii, baada ya mwaka 2008 Sheikh Mansour kuinunua klabu hii na kutumia zaidi ya £ 1 billioni katika kuijenga upya timu kwa kununua wachezaji, mishahara, kukarabati uwanja na vifaa vya mazoezi. Mpaka sasa Sheikh Mansour ameshatumia pesa nyingi sana katika kununua wachezaji na mpaka mwisho wa msimu huu wa usajili anakadiriwa kutumia kwa jumla zaidi ya £ 400m.

CHRIS SMALLING ASAINI MKATABA MPYA NA UTD


MANCHESTER UNITED wamempa Chris Smalling mkataba mpya wa miaka 5 baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mwaka wake wa kwanza ndani ya kikosi cha Red Devils. The 21-year old defender alihamia United akitokea Fulham last summer kwa deal la paundi million 7. Na akiwa ameonyesha uwezo mkubwa katika kuisadia United kushinda ubingwa wa 19 wa EPL , amezawadia mkataba huu mnono. Boss Sir Alex aliongea kuhusu mkataba huu mpya wa Smalling na kusema: "Nina furaha sana baada ya Chris kusaini mkataba mpya. Smalling amekuwa mchezaji muhimu tangu ajiunge nasi kutoka Fulham mwaka jana, ana umri mdogo lakini ana kipaji kikubwa, ana nguvu, akili na anajua kuusoma mchezo.Ni hazina kubwa kwa klabu hii." Smalling nae alisema: "Naangalia mbele kudumu na kupata mafanikio ndani ya klabu ya Manchester United".

FIESTA MWANZA TULIONA KIPAJI HIKI

OWEN HARGREAVES AJIKUBALI YUKO FITI KWA KLABU YOYOTE INAYOMTAKA BAADA YA KUA HURU AKITOKEA KLABU YA MANCHESTER UNITED.


Thursday, July 7, 2011

Asamoah, Mwape, Canavaro na Berko wakifanya maandalizi ya mwisho ndani ya BM Executive Barbershop & Beauty Centre kabla ya kuwakabili ST GEORGE.

KAMERA YA BLOG HII IMEWANASA WACHEZAJI WA YANGA ( DAVIS MWAPE RAIA WA ZAMBIA,ASAMOAH KENETH RAIA WA GHANA,NADIR HAROUB 'CANAVARO'-TANZANIA PAMOJA NA GOLIKIPA YAW BERKO RAIA WA GHANA WAKIJIPIGA SOAP SOAP KABLA YA MPAMBANO WAO WA NUSU FAINALI YA KAGAME CASTLE CUP DHIDI YA ST GEORGE YA ETHIOPIA.





Asamoah, Mwape and Canavaro at BM Executive Barbershop Mara baada ya kupata huduma za salon na Massage







Yaw Berko na Davis Mwape mara baada ya kupata huduma ya salon VIP BM Executive Barbershop & Beauty Centre - Kinondoni.












Yaw Berko akipata huduma ya Salon Bm Executive Barbershop & beauty Centre - Kinondoni






Davis Mwape akipata huduma ya salon BM Executive Barbershop & Beauty Centre - Kinondoni






Asamoah, Mwape, Canavaro wakiwa BM Executive Barbershop & Beauty Centre mara baada ya kupata huduma za salon wengine ni Choki na Hassan wafanyakazi wa BM





Asamoah, Canavaro na Mwape wakiwa BM Executive Barbershop & Beauty Centre - Kinondoni kwa huduma za Salon wengine ni Ustadhi na Kulwa wafanyakazi wa BM

WASHAMBULIAJI WAKALI AMBAO HAWAJAWAHI KUTOKEA TANZANIA



1970-1976
Tukiangalia kwa makini historia ya soka la Tanzania kuanzia mwaka 1970 hadi 1976 inaelezwa ndiko walipokuwapo washambuliaji wakali walioweza kufanya vema katika timu zao na ile ya Taifa, hao wanaongozwa na Gibson Sembuli, Adam Sabu, Kitwana Manara, Abdallah Kibaden, Jumanne Hassan ‘Masimenti’ na wengine ambao waliweza kutoa changamoto ya soka nchini.

Hawa waliweza kufanya vizuri kutokana na vitu vingi, ikiwemo utayari wao kwa mchezo wa soka. Pia ni kipindi ambacho wachezaji walipatikana kutoka mashuleni na mitaani.

Kwa mfano Sembuli aliweza kufanya vizuri kutokana na uwezo binafsi wa kumiliki mpira, kutekeleza kile alichokuwa anaelezwa na kocha kila wakati awapo uwanjani, mwili uliojengeka vema kimichezo kuweza kuhimili shuruba za mabeki wakorofi.

Sembuli anaelezwa kuwa, alikuwa na uwezo wa kukaa na mpira kwa muda mrefu zaidi na kuleta madhara langoni kwa adui wakati wowote awapo uwanjani.

Lakini yatasemwa yote kuhusu washambuliaji wa wakati ule, kubwa zaidi ni akili yao kuzama katika soka zaidi kuliko jambo jingine lolote. Hiki ni kitu pekee kinachoweza kumfanya mchezaji kuwa katika kiwango chake wakati wote.

Kati ya wote aliokuwa akicheza nao wakati huo, Sembuli anatajwa kuwa mshambuliaji bora wa ‘enzi’ zake akiwaacha kina Manara, Kibaden na Masimenti.




1977-1982
Hiki ndicho kipindi zilipochomoza timu nyingi za maeneo yaliyohamasika kisoka kama Coastal Union, African Sports, Mseto na nyinginezo ambazo zilikuwa na wachezaji mahiri walioweza kutandaza vema kabumbu.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Mohamed Salim (Coastal), Thuwen Ally (Simba), Peter Tino (African Sports), Omar Hussein (Mseto-Yanga), George Kulagwa, Rashid Hanzuruni na wengineo.

Ndani ya kipindi hiki timu zilizoweza kutoa wachezaji wengi kwa timu ya taifa ni Simba na Pan African pekee. Ikumbukwe kuwa, Pan ilipata uhai baada ya baadhi ya wachezaji kujiengua kutoka Yanga na kuunda timu hiyo.






1982-1985
Baada ya Tanzania kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980, wachezaji wengi kwa ridhaa yao waliachana na soka, hivyo kutoa nafasi kwa wanasoka wengine kujitokeza katika timu mbalimbali.

Miongoni mwa nyota wapya waliojitokeza ni Innocent Haule, Madaraka Selemani, Makumbi Juma, Richard Lumumba, Juma Mgunda, Zamoyoni Mogela, Gebo Peter, Malota Soma bila ya kumsahau mchezaji aliyekuwa kinda wakati huo Edward Chumila ‘Edo Boy’.

Kizazi hiki kinaelezwa kupokea vema kijiti kutoka kwa kaka zao wa 1977-1982, nguvu ya kampuni na mashirika mbalimbali ya umma iliweza kuwafanya waonekane bora katika soka wakati huo.

Katika kipindi hiki, unaweza kukumbuka jinsi kina Edo Boy walivyoweza kuinusuru Simba isishuke daraja baada ya kuwa katika hali mbaya kufuatia kufanya vibaya kwenye Ligi Daraja la Kwanza—Tanzania Bara.

Hiki ni kipindi ambacho wachezaji hawakuwa na shaka juu ya maisha yao kwani fedha kutoka katika mashirika waliyochezea ziliweza kuwainua kimaisha; pia hakukuwapo na tamaa ya fedha miongoni mwao bila kuwajibika kwanza.

Ni kipindi ambacho, timu kama Majimaji, Pamba, Coastal Union na African Sports ziliweza kuchomoza.




EDIBILY LUNYAMILA AKIWA NA MOHAMED HUSSEIN.


1985-1991
Ndani ya kipindi hiki hakukuwapo na wachezaji wengi sana waliojitokeza, zaidi ya wale waliovuma katika kipindi cha 1982-1985 kuendelea kusakata soka, lakini kwa kiasi kikubwa utawala wa Simba na Yanga katika soka uliweza kupungua kidogo.

Timu za Majimaji, Pamba, African Sports, CDA, Tukuyu Stars, Bandari na nyinginezo ziliweza kufanya vizuri katika ligi na kuonyesha msisimko mpya, lakini nyingi ya timu hizo zikipata msaada mkubwa kutoka kwa mashirika yaliyokuwa yakizimiliki.

1991 – sasa
Hiki ndicho kizazi asilia cha soka; kimeweza kupotea na kutuletea wachezaji wachache ambao mpaka leo wangali wanajaribiwa kuweza kuwa na mshambuliaji wa kuisaidia nchi.

Mwanzoni mwa 1991, wakongwe kama Mogela, Madaraka na Edo Boy waliweza kushirikiana na chipukizi kama Nteze John, Edibily Lunyamila, Thomas Kipese, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Dua Said, Said Sued ‘Scud’, Mao Mkami, Fumo Felician, Kitwana Suleiman, Beya Simba na wengineo kuleta changamoto katika nafasi za ushambuliaji miongoni mwa timu zao, lakini hali haikuwa kama zamani.

Baadaye kidogo kikaja kizazi cha kina Maalim Saleh, Nonda Shaaban ‘Papii’, Clement Kahabuka, Bitta John, Victor Bambo na wengineo ambao walionekana kama watu wa kupita wasiokuwa na malengo ya kufika; badala yake wakaendelea kutoa nafasi kwa kina Lunyamila, Madaraka, Nteze, Edo Boy na wengine kuendelea kutamba.

Baadaye kidogo kikaja kizazi cha kina Athuman Machupa, Athuman Macheppe, Emmanuel Gabriel, Abdallah Juma, Monja Liseki, Akida Makunda, Steven Mapunda ‘Garincha’ na baadhi yao kidogo, lakini hawakuweza kufikia uwezo na kasi ya kina Sembuli, Mogela na hata Mohamed Salim.

Ikumbukwe ya kuwa hicho ndicho kipindi ambacho wafanyabishara walijitokeza kwa wingi kudhamini timu mbalimbali ili ziweze kufanya vizuri, bado baadhi ya wachezaji wa wakati huo wangali wanacheza soka hadi leo hii.

MTOTO WA NYOKA NI NYOKA...

Alli Abdallah Kibaden mtoto wa kocha wa siku nyingi nchini Tanzania ambaye kwa sasa anachezea timu ya soka ya watoto ya Convetry City ya England wa tatu kushoto waliosimama.

OKWI AENDA KUFANYIWA VIPIMO KAIZER CHIEFS


Mshambuliaji wa Uganda “Cranes” na Simba ya Tanzania Emmanuel Okwi anakaribia kukamilisha usajili wake kutoka Msimbazi kuelekea katika klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini.

Okwi ambaye bado ana mkataba wa kuichezea klabu yake ya Simba amekuwa kwenye rada za moja ya klabu kubwa kusini mwa afrika, anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo na endapo atafaulu atasaini mkataba ambao utaoiingizia akaunti ya Simba donge nono kama ilivyokuwa kwa wachezaji Mbwana Samatta na Patrick Ochan waliouzwa fedha zaidi ya shilingi mil. 300.

JOSEPH OWINO MAISHA NJE YA SOKA


Beki wa kimataifa wa Uganda aliyekuwa anaichezea klabu ya Simba msimu uliopita Joseph Owino ameongea nab log hii kuelezea maisha yake nje ya soka.

Owino ambaye recently alifanyiwa operation ya goti nchini India kwa sasa yupo kwao nchini Uganda akijiendeleza na elimu huku akijishughulisha na biashara katika kuhakikisha hayumbi kimaisha.

“Nashukuru mungu naendelea vizuri na goti langu, na kwa sasa natumia muda wangu kuwa nje ya uwanja kujiendeleza kielimu, nachukua masters ya Business Administration @Makerere University, na vilevile najishughulisha uuzaji wa ujumla wa vifaa vya stationery.-Owino

JOHN O'SHEA ANAFANYIWA VIPIMO @ SUNDERLAND


Baada ya jana Wes Brown kwenda North East kufanyiwa vipimo na kukamilisha deal la kuhamia Sunderland. Leo mchezaji mwingine kutoka Man United, the versatile John O’shea ameelekea Stadium Of Light kufanyiwa vipimo.

Ikiwa O’shea na Brown watafanikiwa kufaulu vipimo na kujiunga na Sunderland, kocha Steve Bruce atakuwa ametimiza usajili wa wachezaji nane ndani ya kipindi hiki cha usajili , huku Darren Gibson nae akiwa njiani kujiunga na Black Cats.

Wednesday, July 6, 2011

EXCLUSIVE: JERRY TEGETE NJIANI KUELEKEA MSIMBAZI

"CHUKUA JEZI YA UKWELI HII" JERRY TEGETE AKIWA NA ULIMBOKA MWAKINGWE.

Kutothaminiwa na viongozi na kutopata nafasi ndani ya kikosi cha timu yake kumefungua milango ya klabu ya Yanga kwa mshambuliaji Jerryson Tegete.

Habari kutoka chanzo cha habari kilicho karibu na viongozi wa klabu ya Simba na Tegete zinasema kwa zaidi ya 60% mtoto wa meneja wa uwanja wa CCM Kirumba atakuwa mchezaji wa klabu ya Simba muda wowote kutoka sasa.

Tegete ambaye katika michuano inayoendelea ya CECAFA Kagame Cup anaonekana kuporwa na namba na washambuliaji Asamoah, Hamis Kiiza na Davis Mwape hali ambayo imemkosesha amani mshambuliaji huyo.

NINI YANGA KURUDIA KUPIGA PENALTY MARA MBILI, PENALTY HII IMERUDIWA MARA SITA KUPIGWA!!!!

TARATIBU NA SHERIA ZA KUPIGA PENATI

PENALTY SHOOT-OUT

"Penalty shoot out" ni mipigo ya mpira kutoka kwenye alama maalum iliyowekwa katika "Penalty Box" ya uwanja wa mpira wa miguu.

Hii ni njia inayotumika katika sheria za mchezo wa soka zinazotumika kuamua ni timu gani isonge mbele kwenda hatua inayofuata katika michuano au kushinda michuano.

Mipigo hii ya penati inasimamiwa na sheria na kanuni ambazo zimewekwa na FIFA.




  • TARATIBU ZA KUPIGA PENATI

    *Timu ya kwanza kupiga mkwaju wa kwanza kuamuliwa kwa kurushwa shilingi na rafa ataamua ni goli lipi litumike kwa kupigia penati.

    *Mikwaju yote ya penati itapigwa katika goli moja ili kuhakikisha wapigaji wa penati na magolikipa wote wanakutana na hali yoyote isiyokuwa ya kawaida (kama ikiwepo).

    *Wachezaji wote isipokuwa mpigaji na magolikipa wanapaswa kubakia katikati ya uwanja.

    *Mipigo yote inatakiwa kupigwa kutokea katika alama ya kupigia penati, huku golini kukiwa na golikipa wa timu tofauti na mpigaji.Kipa anatakiwa kubaki katikati ya milingoti miwili huku akiwa amesimama katika mstari wa goli mpaka pale mpira utakapokuwa umepigwa, ingawa anaweza kurukaruka, kunyoosha mikono, kwenda upande mmoja mpaka mwingine akiwa ndani ya mstari wa goli.

    *Kila mpigaji anaweza kupiga mpira mara moja tu, ikiwa mpira aliopiga utazuiwa na golikipa, ukigonga mwamba mpigaji haruhusiwi kuupiga tena (lakini hii ni tofauti ni penati za ndani dk 90).

    *Hakuna mchezaji wa timu ya mpigaji anaruhusiwa kuugusa mpira.

    *Mpira unaweza kumgusa golikipa, milingoti ya pembeni na wa juu kwa idadi yoyote.

    Hali kama hii iliwahi kutokea katika mechi ya fainali za kombe la dunia mwaka 1986-Mexico katika mechi ya Brazil vs France, mechi ambayo iliamuliwa kwa mikwaju ya penati.Wakati wa kupiga penati mchezaji wa Ufaransa Bruno Bellone alipiga mkwaju ambao uligonga mwamba na kurudi uwanjani kisha ukarudi na kuingia golini.Mwamuzi Loan Igna akaamuru kuwa ni goli na nahodha wa Brazil Edinho alipopinga kuwa mpira ulipogonga mwamba na kurudi uwanjani ilitakiwa iamuriwe kuwa tayari France wamekosa akapewa kadi, lakini mwaka 1987 International Football Association Board walithibitisha kuwa kupitia sheria namba 14 inayohusu upigaji wa penalty kuwa maamuzi ya refa yalikuwa sahihi.

    *Ikiwa baada ya mipigo mitano kukamilika na timu zote zikalingana kwa idadi ya magoli, basi zitaanzwa kupigwa penati moja moja kwa kila timu mpaka timu moja itakapofunga na nyingine ikakosa.

    • *Wachezaji 22 pekee waliokuwepo ndani ya mchezo mpaka ulipomalizika ndio wanaruhusiwa kushiriki katika kupiga penati.
    • *Timu inaweza kumbadilisha golikipa ambaye atakuwa ameumia kipindi cha upigaji wa penati, ikiwa timu husika itakuwa haijamaliza idadi ya wachezaji wanaopaswa kubadilishwa.
    • *Ikiwa golikipa atapewa kadi nyekundu, mchezaji mwingine aliyekuwepo ndani uwanja kabla ya mpira kumalizika atachukua jukumu la kukaa golini.
    • *Ikiwa mchezaji mwingine isipokuwa golikipa akiumia au kupewa kadi nyekundu, mikwaju ya penati itaendelea bila kuwepo na mabadiliko yoyote.
    • *Mchezaji yoyote anaweza kuchukua majukumu ya golikipa aliyetolewa kwa kuumia au kwa kadi, na sio lazima mchezaji yuleyule adake mipigo yote anaweza akabadilishwa.
    • *Hakuna mchezaji anayeruhusiwa kupiga penati mara mbili kupigia mpaka pale mzungumko wa wachezaji wote wa timu husika watakapokuwa wamemaliza kupiga mpigo wa kwanza, akiwemo golikipa.
    • *Ikiwa itatokea hali ya ulazima kwa wachezaji kupiga penati kwa mara ya pili (kwa sababu kumekuwa na usawa wa matokeo mara ambapo wachezaji wote halali watakapokuwa wamemaliza mipigo yao ya kwanza) timu hazina ulazima wa kurudia wachezaji wale wale waliowatumia katika penati za 5 za kwanza.
    • *Ikiwa katika mwanzo wa upigaji penati timu moja itakuwa na wachezaji wengi uwanjani tofauti na nyingine, basi timu ambayo imebakiwa na wachezaji wengi uwanjani itabidi ichague mchezaji au wachezaji ambao watakuwa na idadi sawa na wapinzani wao.Mfano, ikiwa timu Team A itakuwa na wachezaji 11 lakini Team B ina wachezaji 10, basi Team A itabidi imchague mchezaji mmoja ambaye hatahusika kabisa na zoezi la upigaji penati hivyo golikipa hawezi kuchaguliwa kuondolewa katika listi ya wachezaji kumi wataohusika na kupiga penati huku akiendelea kudaka.Hatua inahusika ikiwa tu wachezaji/mchezaji alitolewa nje kwa kuumia au kwa kadi ndani ya dakika za kawaida za mchezo na sio ndani ya kipindi cha upigaji penati.